Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa
Botswana Ian Khama amemtaka mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu
mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia
Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana
na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
''Ni wazi
kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa
kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo''.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema
mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku
wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa
Zimbabwe.
Khama
anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula
miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda
mrefu. BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment