Mwakilishi
wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO),Dkt Richard Banda
aliyesimama, akizungumza wakati wa kukabidhi dawa za kutibu maji, wa
kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwangilia Injinia
Mbogo Mfutakamba,na wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya StephanoKiberiti na wa mwisho kulia ni Mkurungezi
Msaidizi TAMISEMI Eng.Enock Nyanda.
Katibu
Mkuu Mfutakamba akitia saini baada ya makabidhiano ya Dawa hizo za
kutibu maji,huku zoezi hilo likishuhidiwa na Mwakilishi wa Shirika la
Afya Ulimwenguni (WHO),Dkt Richard Banda na Mkurungezi Msaidizi TAMISEMI
Eng.Enock Nyanda.
Katibu
Mkuu Mfutakamba wa kulia akibadilishana hati za makabidhiano na
Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO),Dkt Richard Banda.
Na Sheila Simba,Maelezo.
Serikali
kupitia Wizara ya Maji na Umwangiliaji, imepokea mchango wa dawa za
kutibu maji aina ya (calcium hypochlorite) kiasi cha kilogramu 49,500
kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zitakazo sambazwa kwa mamlaka
ndogo za maji nchini.
Akipokea
dawa hizo leo Jijini Dar Es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia
Mbogo Mfutakamba, alisema kuwa dawa hizo zitasambazwa kwenye Halmashauri
mbalimbali kama mchango wa shirika hilo katika kuhakikisha upatikanaji
wa maji safi na salama.
“Naziagiza
Halmashauri na Mamlaka za maji kote nchini ambazo zimeainishwa kupatiwa
dwa hizo kuzitumia kwa usahihi ili kukidhi lengo lililokusudiwa”alisema
Ameeleza
kuwa serikali imejiwekea malengo ifikapo mwaka 2020 kuhakikisha asilimia
85 wananchi wanaoishi vijijini wanapata majisafi na salama na asilimia
90 ya wananchi waishio mijini wanapata huduma hiyo muhimu.
Amesema
kuwa dawa hizo zitasambazwa kutokana na uhitaji wa maji katika eneo
husika na kutoa mfano wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga ambayo imepata
mapipa sitini kutokana na kuzalisha maji mengi.
“Serikali
itaendelea kuchangia katika mamlaka za maji ili kuwapatia watu majisafi
ili kuondoka na tatizo la kipindupindu katika baadhi ya maeneo”alisema
Mfutakamba
Akitoa
shukurani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania Katibu Mkuu huyo Injia
Mfutakamba,amesema kuwa WHO ni shirika la mfano wa kuigwa na wadau
wengine kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwapitia wananchi
majisafi na salama.
Kwa
upande wake mwakilishi wa (WHO) Dkt Richard Banda alisema kuwa dawa hizo
zitasaidia katika kusafisha maji na ili kusaidia jamii kupata maji safi
ya kunywa.
“WHO
tutaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutokomeza,magonjwa
yanayosababishwa na utumiaji wa maji ambayo sio salama”alisema Banda. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment