Rais Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais
Rais
Barack Obama amemtaja Donald Trump "wa ajabu" na "asiye na ufahamu"
baada ya mgombea huyo wa Republican kusema kuwa rais wa Urusi Vradimir
Putin ni kiongozi mzuri zaidi kuliko Obama.
Akizungumza
Laos, Bw Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika
kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais.
Katika
kipindi cha televisheni siku ya Jumatano, Bw Trump alimsifu Bw Putin
kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha
asilimia 82% cha uwezo huo.
Bw Trump alimsifu Bw Putin kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha asilimia 82% cha uwezo huo
Bw Trump na hasimu wake Hillary Clinton walikuwa wakijibu maswali kutoka kwa wanajeshi wa zamani.
Rais Obama alisema: "sidhani kama ana uwezo wa kuwa rais wa Marekani na kila anapozungumza, suala hili linathibitika."
Rais huyo
wa Marekani alielezea kuhusu kazi ya kidiplomasia aliyokabiliana nayo
katika mikutano yote wa Asean na Laos pamoja na ule wa awali wa G20
nchini Uchina.
Alisema :
"Siwezi kukuelezea yote kuhusu mazungumzo niliyokuwa nayo katika
kipindi cha siku nane siku tisa zilizopita na viongozi wa kigeni kwamba
hii ni kazi''.
"
Unapaswa kufahamu ni nini unachokizungumza, lazima kwanza ufanye kazi ya
kuelewa mambo. Unapoongea , lazima kile unachokiongea kiwe kinafanana
na sera unayofikiria unaweza kuitekeleza'' Alisema Obama.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment