Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016.
Serikali
ya Sudan Kusini imekubali Jumapili hii kutumwa kwa askari wa kulinda
amani 4,00 wa ziada nchini mwake, serikali imebaini katika tangazo
lililoandikwa kwa pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini
Juba.
Hivi karibuni, Rais Salva Kiir alikataa katu katu kuwepo kwa askari wa kulinda amani 4,000 wa ziada nchini Sudan Kusini.
Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa Jumamosi hii Agosti 3, lilitoa wito kwa
serikali ya Sudan Kusini kuacha upinzani wake kuhusu kupelekwa kwa
kikosi cha kikanda cha kuimarisha ulinzi katika ujumbe wa askari wa
Umoja wa Mataifa wanaolinda amani katika nchi hiyo inayokumbwa na vita
vya wenyewe kwa wenyewe.
Mabalozi
kutoka nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
walikutana na Mawaziri waandamizi wa serikali mjini Juba na wote
walizungumzia kuunga mkono pendekezo la kutumwa kwa wanajeshi 4,000 wa
ziada kwa kikosi cha askari 13,000 wa UNMISS waliomo nchini humo.
Balozi wa
Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power baada ya kuwasili mjini
Juba, alisisitiza kwamba askari 4,000 wa ziada wa kulinda amani kutoka
Afrika wanahitajika.
Muswada
wa kikosi hiki cha ulinzi ulianzishwa na nchi za Afrika Mashariki, na
majina ya Kenya, Rwanda na Ethiopia yameendelea kutajwa kwa wiki kadhaa
kama nchi ambazo ziko tayari kuunda kikosi hiki.
Mapigano
makali ya Julai 8 hadi 11 katika mji wa Juba kati ya wanajeshi wa rais
Salva Kiir na wale wa kiongozi wa zamani wa waasi, Riek Machar
yamesababisha hali ya usalam kuwa tete nchini Sudani kusini.
Mapigano
haya ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi
kujeruhiwa, yalipelekea Riek Machar kukimbilia uhamishoni. Bw Machar
alikua aliiombajumuiya ya kimataifa kuimarisha tume ya Umoja wa Mataifa
nchini Sudan Kusini (UNMISS), akibaini kukosa uwezo wa kulinda raia
mwezi Julai.RFI
SHARE








No comments:
Post a Comment