Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole baadhi ya majeruhi wa tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani Kagera wakati alipotembelea hospitali ya mkoa
wa Kagera mjini Bukoba Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole baadhi ya majeruhi wa tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani Kagera wakati alipotembelea hospitali ya mkoa
wa Kagera mjini Bukoba Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wafiwa wakati alipokwenda mjini
Bukoba Septemba 11, 2016 kukagua athari za tetemeko la ardhi na
kuwafariji majeruhi, wafiwa na wananchi wa mkoa wa Kagera. Alikuwa
katika Ibada ya kuwambea marehemu hao kwenye uwanja wa Kaitaba .(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu walipoteza
maisha kutokana na tetemeko la ardhi mkoani kagera katika ibad maalum
ya kuwaombea marehemu hao iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyufa zililizosababishwa na tetemeko la
ardhi mkoani Kagera wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nyakato
kuona athari za tetmeko hilo Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyufa zililizosababishwa na tetemeko la
ardhi mkoani Kagera wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nyakato
kuona athari za tetmeko hilo Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya
Nyakato mkoani Kagera wakati alipokwenda shuleni hapo Septemba 11,
2016 kujionea athari za tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipita mbele ya bweni la shule ya sekondari ya
Ihungo mkoani Kagera ambalo liliporomoka kutokana na tetemeko la ardhi
lililoukumba mkoa huo . Alikuwa katika ziara ya kukagua athari za
tetemeko hilo na kuwapa pole wananchi, Septemba 11, 2016.(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba
mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi
lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.
Tetemeko
hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine
253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada
ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo
44 ya taasisi mbalimbali za umma.
Kufuatia
tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John
Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea
kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.
“Poleni
sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni
mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu Serikali
ipo pamoja nanyi na haitawatupa mkono,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu
itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya
tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona
namna ya kuwasaidia waathirika.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za
haraka kwa kuwatafutia eneo salama la kulala wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote yameathirika na tetemeko hilo
na hayafai kutumika.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna
mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi
kulala uwanjani.
Pia
Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia
kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze
kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.
Naye Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa
wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao
zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari
zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Awali
Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170
wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone
haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali
kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment