Mchezaji
wa Kinondoni Hassan Kipera (nyekundu) akimiliki mpira mbele ya mchezaji
wa Mbeya Ernest Kamange wakati wa fainali za taifa za mashindano ya
Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
Mchezaji
wa Kinondoni SalumYohana (nyekundu) akijiandaa kuifungia timu yake bao
la pili wakati wa fainali za taifa za mashindano ya Airtel Rising
Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Kinondoni ilishinda 2-1.
Mchezaji
wa Kinondoni Salum Yohana (nyekundu) akimpiga chenga mlinda mlango wa
Mbeya ma kuifungia timu yake bao la pili wakati wa fainali za taifa za
mashindano ya Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume
jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
Beki
wa Kinondoni Haji Mohammed Haji (nyekundu) akipinga mpira kichwa
kuondoa hatari golini kwake huku akisongwa na washambuliaji wa Mbeya
wakati wa fainali za taifa za Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye
uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
Mshambuliaji
wa timu ya Mbeya (nyeupe) akichuana vikali na beki wa timu Kinondoni
wakati wa fainali za taifa za Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye
uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa
atakuwa mngeni rasmi wakati wa kufunga fainali za taifa za michuano ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Jumapili 11
Septemba mwaka huu kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Salum Madadi amesema hiyo
ni heshima kubwa kwa vijana, viongozi na wadhamini wa mashindano hayo.
“Ujio wa Waziri Mkuu utaamusha ari ya wachezaji”, alisema Madadi.
Fainali
za mashindano hayo zilifunguliwa Jumanne 6 Septemba na Mkuu wa wilaya
ya Ilala Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda. Jumla ya timu 12 zinashiriki mashindano hayo huku sita zikiwa
za wavulana na sita wasichana. Mikoa inayoshiriki niTemeke, Ilala,
Kinondoni, Mbeya, Morogoro na Mwanza kwa wavulana na Temeke, Ilala,
Kinondoni, Arusha, Lindi na Zanzibar kwa wasichana.
Katika
hatua nyingine, timu za mkoa wakisoka wa Kinondoni za wavulana na
wasichana zimekuwa za kwanza kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya
Airtel Rising Stars baada ya mechi zilizochezwa asubuhi, Alhamsi
Septemba 8 kwenye uwanja wa Karume. Timu ya wasichana Kinondoni
waliwafunga Lindi 10-0 huku wavulana wakishinda 2-1 dhidi ya Mbeya.
Wasichana
Kinondoni walianza vyema mashindano hayo baada ya kuwafunga Arusha 4-0,
kwa hivyo waliingia uwanjani wakiwa wakitaka sare ya aina yeyote
kutinga hatua ya nusu fainali. Iliwachukua dakika tano kupata goli la
kwanza likifungwa na Aisha Juma. Mchezaji nyota wa mechi hiyo Prisca
Bahela aliifungia timu yake mabao matano peke yake kati ya dakika ya 16,
20, 25 kipindi cha kwanza na 30 na 31 kwenye kipindi cha pili.
Magoli
mengine yalifungwa na Isabela John dakika ya 7 na 19 kipindi cha kwanza
huku Mwantum Ramadhani na Veronica Mapunda wakifunga dakika ya 23 na 29
kipindi cha pili.
Kwenye
mechi kati ya wavulana Kinondoni na Mbeya, timu hizo ziliingia uwanjani
kila moja ikiitaji ushindi ili kusonga mbele. Hali hiyo ilisababisha
mechi kuwa kali na ya kuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.
Timu
ya Kinondoni ndio iliyokuwa ya kwanza kupata goli kwenye dakika ya 14,
goli likifungwa na Shaban Maguli aliyewashinda nguvu mabeki wa Mbeya na
kuruka juu kufunga akiunganisha krosi nzuri kutoka kwa mshambualiaji
mwenzake Marco Muhiru. Baada ya kupata bao, kasi ya mchezo iliongezeka
huku Mbeya wakitafuta goli la kuzawazisha na Kinondoni wakitaka kuongeza
bao kujihakikishia ushindi. Mpaka kipindi kwa kwanza kinamalizika
Kinondoni 1 Mbeya 0.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi ileile lakini walikuwa ni Kinondoni
waliowafurahisha mashabiki wake kwenye dakika ya 57 baada ya kiungo
Salum Yohana kupokea pasi nzuri kutoka kwa Hassan Kipera na kufanya kazi
nzuri ya kuwachambua mabeki watatu pamoja na mlinda mlango na
kuiandikia timu yake bao ya pili.
Baada
ya bao hilo, Mbeya waliongeza kasi iliyosababisha kupata bao dakika ya
77 likifungwa na Pius Crinton akiunganisha mpira wa kona uliopingwa na
Ernest Kamange. Matokeo yalibakia hivyo mpaka mwisho wa mechi na kufanya
Kinondoni wavulana na wasichana kusonga mbele.
Robo fainali za michuano hiyo zitachezwa Jumamosi Septemba 10 huku zikihitimishwa na kilele cha fainali Jumapili 11 Septemba.
SHARE
No comments:
Post a Comment