Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa taarifa ya wilaya kwa Waziri
Waziri Prof.Ndalichako akiwapongeza Viongozi wa Wilaya ya Kasulu kwa kubuni mkakati endelevu wa elimu
Waziri Prof.Ndalichako na DC Kanali Mkisi wakikagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu
Waziri Prof.Ndalichako akitoa akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi
Waziri Ndalichako na Kanali Mkisi wakikagua ufanyaji wa mitihani katika shule ya msingi Mwenge,Wilayani Kasulu mkoani Kigoma
Na Abel Daud-Globu ya Jamii Kigoma
Waziri wa
Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako amewahakikishia
wanafunzi kote Nchini kwamba Serikali ya awamu ya tano imejipanga
kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki ili kila atakaye faulu aweze
kuendelea na hatua ya juu zaidi ya kielimu.
Hayo
ameyasema leo hii Wilayani Kasulu alipotembelea Shule ya Msingi Mwenge
pamoja na Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu kukagua miundombinu tayari kwa
kupokea wanafunzi wa diploma kutoka UDOM.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi amemueleza
Waziri Ndalichako kuwa Wilaya yake imejipanga kuinua elimu kwa kiwango
kikubwa na kuwataka watumishi wa halmashauri za Kasulu pamoja na
wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano ili kufikia malengo waliyojipangia
ya kuinua elimu wilayani hapo.
Prof.Ndalichako
ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kasulu kwa kubuni mkakati endelevu wa
kuinua elimu wilaya ya kasulu na kuwataka kusimamia swala hilo kwa
vitendo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment