Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
Serikali
imeanza mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya China kwa ajili ya
kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati Afrika ikiwemo Tanzania.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba alipokuwa akijibu swali la Mhe.
Munde Tambwe lililohusu mkakati wa Serikali kupitia diplomasia ya uchumi
na nchi ya China kuunganisha wajasiriamali wadogo.
Dkt.
Kolimba amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 4 barani afrika
ambazo Serikali ya China imechagua kuwekeza viwanda vyake katika miaka
mitatu ijayo.
Naibu
Waziri huyo ameongeza kuwa, Serikali ya china imeanzisha mfuko maalumu
wa fedha kwa ajili ya kuwezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati wa
afrika ambapo Serikali ya Tanzania imeshafanya mazungumzo na Benk ya
maendeleo ya China.
“Serikali
imeanza mazungumzo na benki ya maendeleo ya china kwa ajili ya
kuwezesha mabenki nchini yaweze kukopa fedha hizo na hatimaye kuweza
kuwakopesha wajasiriamali wetu wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya
viwanda kwa kushirikiana na wenzao wa china,” alifafanua Dkt. Kolimba.
Aidha,
amesema kuwa matarajio ya Serikali ni kuona mabenki nchini yanakidhi
vigezo na masharti ya kuchukua fedha kutoka Mfuko wa China ili
watanzania waanze kupata mitaji mapema iwezekanavyo.
Mbali na
hayo Balozi wa Tanzania nchini China umekuwa ukishawishi wafanyabiashara
kutoka china kuwekeza nchini nan a kuandaa ziara za makampuni
mbalimbali ya China kutembelea kituo cha uwekezaji (TIC) nchini.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment