![Image result for Azam FC](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMmphP1gyi1Zlg5ARqv0sQ4X2JnEfyxFuVgTu2ZkMmnmuNGouZMTsDgi8JFxRSNaT923MQSLeCwXitSg5S0FE2-fihWJAVHWgSqfV0uIxO1oseuEfEQywazi_kvKRTjzgwqT1SFfiAfr4/s1600/2.jpg)
Na.Alex Mathias
Timu ya
Azam FC inatarajia kutupa karata yake ya kwanza muhimu kwa kucheza na
Kagera Sugar Leo mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa
Kaitaba huku Kocha Mkuu Zeben Hernandez ametamba kuwa watakuwa na kazi
moja tu ya kusaka alama tatu katika kipute hicho.
Akizungumza
amesema kuwa ni mechi nzuri tunayotakiwa kuzoa pointi tatu, hali ya
timu haipo vizuri sana kutokana na matokeo, lakini nafikiria kuwa mechi
ya mwisho tuliyocheza na kupata ushindi ilibadilisha mawazo ya
wachezaji.
“Malengo
yetu ni kuendelea kuboresha kiwango cha timu na kushinda pointi tatu
kesho, kwa sababu nafikiria kuwa mashabiki, wachezaji na Azam FC kwa
ujumla wanahitaji pointi tatu,” alisema Hernandez.
Kocha
huyo wa zamani wa Santa Ursula ya Hispania, aliweka wazi kuwa katika
mchezo huo atawakosa nyota wake watatu ambao ni mabeki Shomari Kapombe,
Bruce Kangwa na kiungo Himid Mao, aliyepata kadi nyekundu kwenye mchezo
uliopita dhidi ya JKT Ruvu.
Azam FC
itaingia kwenye mchezo huo, ikiwa inakamata nafasi ya sita kwenye
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16, hivyo ushindi wowote wa Leo
utaifanya kufikisha jumla ya pointi 19 na kupanda kwa nafasi mbili hadi
ya nne ikizishusha Mtibwa Sugar (17) na wapinzani wao hao Kagera (18).(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment