Mkuu wa kituo cha polisi Kibaya Patrick Kimaro (sabasita) akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Wafanyakazi wa TCRA Kanda ya Kaskazini wakiendesha mafunzo hayo
Mkuu
wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Tumaini Magessa (kulia) na mkuu wa
polisi wa wilaya hiyo Fadhili Luoga wakifutilia mafunzo hayo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Tumaini Magessa amewaasa askari
polisi kuwachukulia hatua kali wahalifu wa mitandao ili kukomesha
matukio hayo ambayo yamekuwa kero kwa jamii katika sehemu tofauti hapa
nchini.
Magessa
alitoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya maofisa wa polisi wilaya
ya Kiteto juu ya masuala ya uhalifu wa mitandao, yaliyoandaliwa na
mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya kaskazini na kufanyika
kwenye jumba la maendeleo ya jamii mji mdogo wa Kibaya.
Alisema
ukuaji wa teknolojia umewezesha kupata mawasiliano ya intaneti kupitia
simu, kutuma na kupokea fedha kwa kutumia simu za mikononi na kulipia
huduma mbalimbali ila baadhi ya watu wanatumia matumizi hayo vibaya
hivyo wachukuliwe hatua kali.
Alisema
maendeleo ya matumizi ya simu yamekuja na changamoto hizo pamoja na
matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano na baadhi ya watumiaji
wameibiwa pesa kwenye akaunti zao za fedha kupitia mitandao.
Meneja
wa TCRA kanda ya kaskazini Annette Matindi alisema kuna aina nyingi za
uhalifu kupitia mitandao ya simu na intaneti ikiwemo kutokusajili laini
za simu au kutumia majina bandia kusajili simu.
Matindi
alitaja makosa mengine ni kutumia simu kutuma ujumbe wa matusi au kasha
na vitisho, utapeli na wizi wa fedha kupitia mtandao na simu ikipoteza
mawasilino kwa muda pindi yakirudi unakuta fedha zimeibiwa.
Mkuu
wa Kituo cha polisi Kibaya, ASP Patrick Kimaro (Sabasita) alitoa wito
kwa jamii kuzingatia na kusisitiziwa kuwa na matendo ya uadilifu ili
kukomesha matukio ya makosa ya mitandaoni kupitia ulimwengu huu wa
teknolojia.
Kimaro
alisema watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapaswa kutambua kuwa
wakitumiwa picha, sauti au maneo ya kashfa, uchochezi au udhalilishaji,
wanapaswa kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili kukomesha hali hiyo.
Alisema
kusambaza picha, sauti au maneno yenye viashiria vya makosa ya mtandao
kwa kisingizio kuwa umetuliwa na mtu hakusababishi mtu asichukuliwe
hatua hivyo wanapaswa kufuta kuliko kusambaza.
Pia,
alisema mafunzo kama hayo yanapaswa kutolewa mara kwa mara kwa askari
polisi ili waendelee kukomesha makosa hayo kwani vijana wengi wenye
utaalamu wa kompyuta na suala la IT wanajifunza mbinu mpya kila mara za ualifu wa mitandao.
Kwa
upande wake, askari wa kituo hicho Bkari Yusuf alisema kwa sababu TCRA
wana uwezo wa kuzima simu feki, pia watu wanaotumia mitandao ya kijamii
kwa kuvunja maadili wanapaswa kufungiwa ili kukomesha makosa hayo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment