Na.Alex Mathias.
Kikosi
cha Azam FC kimepeleka maumivu tena kwa timu ya Kagera Sugara baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
bara uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Wenyeji
walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Themi
Felix dakika ya 32 kutokana uzembe wa mabeki wa wageni hata hivyo
halikudumu kwani kiungo mshambuliaji Mudathir Yahya kusawazisha dakika
ya 40 hadi mapumziko timu hizo zilikwenda nguvu sawa.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kushambuliana alikuwa Themi Felix alifunga la pili
dakika ya 68 kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya Agrey Moris kuunawa
mpira ndani ya 18 baada ya kuingia kwa bao hilo kuliamsha hasira kwa
Azam Fc na kulisakama lango la wenyeji.
Mchezaji
wa zamani wa Yanga,Frank Domayo aliisawazishia timu yake kunako dakika
ya 80 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango na Nahodha wa Azam
alipeleka Maumivu kwa Kagera Sugar, John Bocco kwa kufunga la tatu na la
ushindi dakika ya 86 hadi mpira una malizika Azam FC wameibuka na
ushindi wa magoli 3-2.
Kwa
matokeo hayo Azam FC wamepanda hadi nafasi ya nne wakiwa na alama 19
katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara wakati Kagera Sugar
wameendelea kuugusa maaumivu kwa kufungwa mechi ya pili kwani Mchezo
uliopita walikubali kuchakazwa kwa aibu na Yanga cha magoli 6-2 na
kushuka hadi nafasi ya tano wakibaki na alama 18. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment