Na Daudi Manongi, MAELEZO
Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL) imekusanya shilingi bilioni 8.1 katika robo ya
kwanza ya mwaka 2016 ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 1.6 ya robo ya
kwanza ya mwaka 2015 ambapo ilipata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni
6.5.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw.Masanja Kungu Kadogosa wakati
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Bwana
Masanja anasema kuwa huduma ya usafirishaji abiria imezalisha mapato ya
wastani wa shilingi bilioni 1.1 katika kipindi cha mwaka 2016 na Wastani
wa shehena kwa robo mwaka imeongezeka na kufikia tani 63,251
ukilinganishwa na tani 48,681 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho
mwaka jana.
Aidha
kati ya mwezi Juni hadi Octoba mwaka 2016 kampuni imetekeleza miradi
midogo kadhaa ya kujenga michepuo ya reli kwenda kwenye viwanda vya
wateja wa TRL wenye kuzalisha shehena,ambapo Baadhi ya miradi ya reli za
michepuo zilizojengwa ni kwenda kiwanda cha mbolea cha Yara kilichopo
Kurasini na kiluwa Group ya Mlandizi huku michepuo mingine inatarajiwa
kujengwa kuelekea viwanda vya Saruji vya Rhino na Sungura vilivyopo
mkoani Tanga.
Aidha
Bw.Kadogosa amesema kuwa wamefanikiwa kufanya ukarabati wa mabehewa ya
mizigo 120 yaliyogharimu shilingi milioni 700 na kusema kama
yangefanyiwa ukarabati nje ya nchi yangegharimu shilingi bilioni 26.
Mbali na
hayo menejimenti ya TRL inaendelea kutoa kipaumbele katika kutatua madai
ya wafanyakazi wake ikiwemo kuwasilisha Michango katika mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya(NHIF),WADU na Saccos NMB ambapo baada ya kuwasilisha
makato wafanyakazi wameanza kupata huduma stahiki.
Aidha
malimbikizo ya nyongeza ya mshahara yameshatengewa shilingi milioni 600
ambazo zimelipwa ikiwa ni awamu ya tatu na menejimenti inajipanga
kumaliza awamu nyingine zilizosalia.
Mkurugenzi
huyo ametoa wito kwa wadau na wananchi kuhakikisha wanalinda
miundombinu ya reli na kuripoti mara moja kwenye vyombo vya dola wale
wote wanaohujumu miundombinu kwa manufaa binafsi.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment