Serikali ya China imeitaka Marekani kuimarisha juhudi zake katika kuangazia mgogoro wake na Korea Kaskazini.
Msemaji
wa wizara ya maswala ya kigeni nchini China Geng Shuang amesema kuwa
Washington na Pyongyang zinafaa kuchukua majukumu zaidi katika kuangazia
hali ya wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini huku China
ikiunga mkono juhudi hizo.China hivi majuzi ilipiga marufuku uagizaji wa makaa kutoka Korea Kaskazini hatua inayoonekana kuathiri uchumi unaoyumba yumba wa taifa la Korea Kaskazini.
Hatahivyo rais wa Marekani Donald Trump wiki iliopita alisema kuwa China inawezakufanya mengi ili kutatua swala hilo ikitaka.
SHARE
No comments:
Post a Comment