Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemuonya Rais wa
Burundi Pierre Nkurunziza dhidi ya kugombea muhula wa nne madarakani
akisema hatua kama hiyo itauzidisha mzozo unaoendelea nchini humo.
Guterres amesema anatiwa wasiwasi mkubwa na matamshi ya hivi karibuni
kutoka kwa Nkurunziza yanayodokeza kuwa atagombea muhula wa nne na hivyo
Burundi itahitaji kufanya mageuzi ya katiba ili awanie muhula mwingine.
Akiwasilisha ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Guterres
amesema azma yoyote ya Rais huyo wa Burundi kubakia madarakani kwa
muhula wa nne kutaitumbukiza nchi hiyo katika mzozo zaidi na kuhujumu
juhudi za kutafuta amani. Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la
kushughulikia wakimbizi la UNHCR, Zaidi ya watu laki tatu wameikimbia
nchi hiyo na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia watu nusu
milioni mwaka huu. Nkurunziza amekuwa madarakani tangu mwaka 2005.
DW
DW
No comments:
Post a Comment