Jumamosi
Februari 18,2017,kumefanyika kikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano
Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church
Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye
anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017.
Kikao
hicho kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mamia
ya wachungaji,viongozi na waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga
ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa
Josephine Matiro.
Mnenaji
mkuu katika kikao hicho alikuwa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho Askofu Dkt. Makala aliwapongeza viongozi wa
kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa
kanisa hilo,Mchungaji Jakobo Mapambano kwa kuandaa sherehe ya kumuaga
Askofu Nkola ambaye amekuwa askofu wa Kanisa hilo tangu tarehe
24.10.1993.
Askofu
Makala alitumia fursa hiyo kuwaonya waumini wa kanisa hilo kutokuwa na
tamaa ya madaraka ya uongozi kwa nafasi itakayoachwa na Askofu Nkola
hili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza na kusisitiza kuwa ni vyema
kiongozi atakayeziba nafasi hiyo apatikane kwa utaratibu unaotakiwa.
Akizungumza
wakati wa kufungua kikao hicho,mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa dini
kuongeza nguvu katika kueneza neno la mungu kwani watu wengi katika mkoa
wa Shinyanga bado hawajamjua vyema mungu,wengi wao hawana dini.
Katika
hatua nyingine Matiro aliwaomba viongozi wa dini kuiunga mkono serikali
katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhubiri watu waachane na
vitendo.Mwandishi
mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde,alikuwepo katika kikao
hicho…Ametuletea picha 50 za matukio yaliyojiri katika kikao
hicho…Tazama hapa chini.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasalimia viongozi wa kanisa
la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakati akiwasili katika ukumbi wa NSSF
mjini Shinyanga kuhudhuria kikao chakikao cha kamati ya Maandalizi ya
Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland
Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola
ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017 .Kulia ni Makamu wa
Askofu Dayosisi ya Shinyanga mchungaji Aaron Malyuta
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasalimia viongozi wa kanisa
la AICT Dayosisi ya Shinyanga akisalimiana na wachungaji wa kanisa la
AICT
Ndani
ya ukumbi wa NSSF: Kushoto ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya
Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano,katikati ni mkuu wa wilaya ya
Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala baada ya kuwasili
ukumbini.
Maombi yakiendelea baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini
Wajumbe wa kikao hicho wakisali ukumbini
Katibu
mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano
akitambulisha viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria kikao hichoAskofu
wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga, Dr. John Nkola.Hakuwepo wakati
wa Kikao cha leo(Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog
Katibu
mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano
alisema kikao hicho ni hatua ya awali ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na
sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania
(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye anastaafu
uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017.
mkuu
wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT
Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala
wakimsikiliza mchungaji Mapambano
Katibu
mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano
akiwapungia mkono wajumbe wa kikao hicho kutoka ndani na nje ya mkoa wa
Shinyanga
Makamu
wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron
Malyuta akizungumza wakati wa kuthibitisha tamko la kuwakaribisha
wajumbe na wageni katika kikao hicho
Wajumbe wakiwa ukumbini
Kwaya AICT Shinyanga wakiimba ukumbini
Kwaya ya AICT Shinyanga ikiimba
Wajumbe wakiwa ukumbini
wajumbe wa kikao hicho wakiwa wamesimama
Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akizungumza ukumbini
Kikao kinaendelea
Wajumbe wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti
wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa
Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga
Dkt.John Kanoni Nkola,Erasto Kwilasa ambapo aliwaomba viongozi na
waumini wa kanisa hilo kushirikiana naye katika kufanikisha mkutano huo
na sherehe hizo
Kwaya AICT Kambarage ikiimba
Viongozi
wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa
Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga
Dkt.John Kanoni Nkola wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Kushoto
ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo
Mapambano na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro wakiwa
wamesimama ukumbini
Viongozi wa Kanisa wakiwa ukumbini
Maombi yakiendelea kabla ya Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala
Maombi yanaendelea
Askofu
wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo
aliwataka waumini kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga kuyaenzi mambo
mazuri yote yaliyofanywa na Askofu Dkt. John Nkola
Askofu
wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala pia aliwahamasisha waumini wa kanisa hilo
kudumisha upendo
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza ukumbini
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akiendelea kuzungumza
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akitoa neno ukumbini
Askofu
wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala akiwa amesimama baada ya kumaliza kuzungumza
Meza kuu wakiwa wamesimama,wa kwanza kushoto ni mchungaji Samwel Njile kutoka Kanisa la AICT Pastoreti ya Masumbwe mkoani Geita
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
Maombi yanaendelea
Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akizungumza ukumbini
Mchungaji
Samwel Njile kutoka Kanisa la AICT Pastoreti ya Masumbwe mkoani Geita
akiteta jambo na Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya
Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano
Wajumbe wa kikao
Makamu
wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron
Malyuta akimkaribisha mgeni rasmi,mkuu wa wilaya ya Shinyanga ili
azungumze na wajumbe wa kikao hicho
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini ambapo
aliwapongeza waumini wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga kuandaa
sherehe maalum kumuaga Askofu Dkt. Nkola
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kufikisha
neno la mungu katika maeneo mengi zaidi ili wananchi wawe na hofu ya
mungu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kuzungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na mchungaji Mapambano baada ya kumaliza kuzungumza
Kushoto
ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo
Mapambano,katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala wakiwa ukumbini
Katibu
mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano
akimsindikiza Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala kutoka ukumbini baada ya kikao
hicho kufunguliwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment