Naibu
wa Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwenye
kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa
kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala ili kuona namna
huduma zinavyotikewa.
Ameamua kufanya ziara hiyo
sababu kuna ongezeko kubwa la wateja siku za hivi karibuni kutokana na
kuongezeka udhibiti. Na kuna taarifa kwamba wanaouza dawa za kulevya
(drug dealers) wameathiriwa sana kwa kupoteza mapato ya sh bilioni 70
kwa uwepo wa vituo hivi ambavyo kwa sasa vinahudumia wateja 3351, na
hivyo wameanza kubuni mbinu za kuwarudisha kwenye matumizi ya dawa za
kulevya kwa mbinu mbalimbali ikiwemo kudai kuwa methadone haifanyi kazi.
Dkt. Kigwangalla ameagiza:
1. Hospitali zote za kanda zianzishe vituo vya rehab ndani ya miezi 6
2. Hospitali zote za mikoa nchini zianzishe kliniki ya kutoa methadone ndani ya miezi 6
3. Katibu Mkuu afya ahakikishe
kuna Daktari bingwa wa afya ya akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na
kusimamia vituo vya kutoa tiba ya methadone
4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni aongeze eneo la kliniki sambamba na watumishi kwenye kituo hiki
5. Kamishna wa polisi wa
operesheni maalum afuatilie wateja (exit follow-up) wanaotoka kliniki
ili kudhibiti mkakati wa drug dealers wanaolenga kuwarubuni na
kuwarudisha kwenye dawa za kulevya wateja wa vituo hivi.
Msafara wa Dkt. Kigwangalla umeelekea Temeke Hospitali kwenye kituo kingine kama hiki.
SHARE
No comments:
Post a Comment