Serikali ya Kenya itapiga marufuku matangazo ya serikali katika
vyombo vya habari binafsi, kulingana na taarifa iliyoonekana na shirika
la habari la AFP hapo jana. Hatua hiyo inakuja huku Rais Uhuru Kenyatta
akiwa anajitayarisha kuzindua gazeti la serikali ambalo litakuwa
likisambazwa bure. Kwa mujibu wa Shirika la Matangazo la Serikali,
matangazo ya serikali kwa sasa yanaingiza euro milioni 18 kwa mwaka kwa
magazeti yote nchini Kenya. Barua iliyotoka kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma
Kenya, Joseph Kinyua, imesema baraza la mawaziri limeidhinisha
kuanzishwa kwa gazeti hilo la serikali litakaloitwa MY.GOV ambalo
limesema litaeleza agenda ya serikali kwa njia sahihi zaidi na kuonyesha
jamii jitihada zinazochukuliwa na serikali kuboresha maisha ya wananchi
wake. Shirika lisilo la serikali la kutetea uhuru wa kujieleza la
Article 19 limesema sera mpya ya serikali ya kupiga marufuku matangazo
ya serikali katika vyombo vya habari nchini humo ni njia nyengine ya
serikali kutaka kuthibiti vyombo vya habari binafsi nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment