Mwandishi wa habari kwa gazeti la Ujerumani la Die Welt, Deniz Yucel,
amewekwa jela kwa amri ya Mahakama ya Kituruki iliyotolewa jana, huku
akisubiri kesi yake ya madai ya kuhusika na usambazaji wa propaganda za
kigaidi pamoja na uchochezi wa chuki. Hatua hiyo inakuja katika wakati
ambapo Uturuki imegubikwa na ukandamizaji wa waandishi wa habari pamoja
na vyombo vya habari kwa jumla. Yucel mwenye uraia wa nchi zote mbili,
Ujerumani na Uturuki, alikamatwa na polisi Febuari 14 baada ya kuripoti
juu ya shambulio la udukuzi la akaunti ya barua pepe ya waziri wa
nishati wa Uturuki. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema habari
zilizomfikia za kukamatwa kwa Yucel ni za kusikitisha na kukatisha
tamaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment