Timu ya Ujerumani ya Borussia Moechengladbach imefanikiwa kuingia
kwenye timu 16 zitakazo shiriki katika fainali za ligi ya barani Ulaya.
Timu hiyo imefuzu baada ya kuifunga timu ya Italia Fiorentina mabao 4
kwa mawili katika pambano la pili. Wakati huo huo mabingwa wa ligi kuu
ya Uingereza Leicester City wamemuachisha kazi kocha wao Claudio Ranieri
miezi tisa baada ya kuiongoza timu hiyo hadi ilipotwaa ubingwa. Timu
hiyo sasa imebakiwa na pointi moja tu juu ya mstari wa kuteremshwa
daraja huku ikiwa imebakiza kucheza mechi 13.
Thursday, February 23, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment