Rais wa Marekani Donald trump amesema atalitaka Baraza la Congress
kuongeza bajeti ya ulinzi wa nchi kwa asilimia 10, pamoja na kupunguza
bajeti ya misaada ya Marekani kwa nchi za nje. Maafisa wa serikali ya
Trump wamesema kuwa bajeti hiyo ya ulinzi itaongezeka kwa dola bilioni
54, sambamba na hilo bajeti za programu zisizo za kijeshi zitapunguzwa.
Trump amesema mabadiliko hayo ya bajeti yanalenga kutekeleza ahadi zake
za wakati wa kampeni za kuimarisha usalama wa Marekani. Trump pia
ameahidi kujenga ukuta katika mpaka wa kati ya Mexico na Marekani,
kuwafukuza wahamiaji haramu nchini pamoja na kuwaangamija wanamgambo wa
makundi ya kigaidi.
Tuesday, February 28, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment