Makundi kadhaa ya Kiyahudi pamoja na shule za Kiyahudi zameripoti
vitisho vya ulipuaji wa mabomu katika majimbo 11 nchini Marekani, siku
moja baada ya zaidi ya makaburi 100 ya Wayahudi kuharibiwa. Baraza la
Congress la Wayahudi Duniani limelitaja tukio hilo kuwa linaashiria woga
na dharau. Vitisho hivyo vya ulipuaji wa mabomu ambavyo vyote
vilithibitishwa kuwa ni vya mzaha, vilitokea jimbo la Alabama, Delaware,
Florida, Indiana, Maryland, Michigan, New Jersey, New York, North
Carolina, Pennsylvania na Virginia. Katika baadhi ya vituo hivi ni mara
ya pili au ya tatu ndani ya mwaka huu, ambapo walilazimika kujitayarisha
kukabili vitisho vya aina hiyo. Baraza la Wayahudi limeitaka polisi ya
Marekani, kuchukua hatua zinazostahili haraka iwezekanavyo kuwakamata
wanaohusika na vitisho hivyo ambavyo wamesema vina nia ya kusambaza hofu
na wasiwasi katika jamii za Wayahudi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment