Julian Msacky
KAMA kuna mgororo unaisumbua dunia kwa muda mrefu bila kupata
ufumbuzi ni wa Israel na Palestina.
Umoja wa Mataifa (UN) umesalimu amri. Mataifa ya Magharibi
yanaugusagusa na kuacha ulivyo.
Ni sawa na mfupa uliomshinda fisi. Swali sasa ni je, nani atamaliza mzozo huo? Ni viongozi wa kiserikali au dini?
Ni sawa na mfupa uliomshinda fisi. Swali sasa ni je, nani atamaliza mzozo huo? Ni viongozi wa kiserikali au dini?
RAIS DONALD TRUMP
Je, UN na mataifa mengine yataendelea kuangalia namna Wapalestina na Waisrael wanavyonyukana kila mara?
Je, UN na mataifa mengine yataendelea kuangalia namna Wapalestina na Waisrael wanavyonyukana kila mara?
Historia inaonesha kuwa mgogoro huo umejikita katika masuala
ya kidini hivyo ufumbuzi wake ni utata mtupu.
Tunaambiwa kuwa wakati Waisrael wakiwa utumwani Misri kuna
nchi ilikuwa na asali na maziwa.
Nchi hiyo (Palestina?) ilikuwa na kila kitu, inapendeza,
yenye rutuba na hakika ilikuwa ni kama paradiso.
Walipokuwa nchini Misri wana wa Israel walilalamika kuteswa
hivyo wakamlilia Mungu ili awaokoe.
Mwenyezi Mungu akafanya hivyo kwa kumtumia Nabii Musa na kwa
mkono wa Mungu aliwaondoa Misri.
Baada ya kufanya hivyo aliwaongoza Waisrael kwenda nchi ya
ahadi.
Wakiwa tena njiani walipata mateso makali jangwani na shida
zilipozidi walitamani Musa awarudishe Misri.
Mateso yalipokolea Waisrael waliamua kujitengenezea miungu ya
shaba na kumweka pembeni Mungu wao.
Mwenyezi Mungu alichukizwa na tabia hiyo na kuvunja agano na
wana wa Israel licha ya kuwa ni taifa teule.
Kadri siku zilivyosogea umri wa Musa nao ulisogea na
alipofikisha miaka 120 alifariki dunia. Hakuona nchi ya ahadi.
Kwa sababu hiyo Waisrael walibaki wakirandaranda jangwani
hadi nabii Joshua alipochukua nafasi ya Musa.
Hii ilikuwa ni safari ndefu yenye majaribu mengi ili kupima
imani ya Waisrael kwa Mwenyezi Mungu.
Hakuna mwenye jibu la moja kwa moja kama yupo kiongozi wa
kisiasa au dini anayeweza kuleta amani maeneo hayo.
Amani ya kweli itapatikana endapo haki isipotamalaki na
mkubwa kumheshimu mdogo ili kuondokana na mapambano ya Goliathi na Daudi
Bila kufanya hivyo Wapalestina wataendelea kujihami kwa kila
mbinu ili kuzuia uvamizi katika ardhi yao.
Kama zilivyo nchi nyingine Palestina inahitaji kutambuliwa na
kupewa hadhi badala ya kunyanyapaliwa.
Kauli ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
kwamba:
“Katika makubaliano yoyote ya amani, Israel lazima iwe na
uwezo wa kudhibiti usalama katika eneo lote la Magharibi mwa mto Jordan”.
Eneo hilo linahusisha ukingo wa Magharibi na ni kitovu cha
taifa la Palestina linalotarajiwa kuundwa kulingana na makubaliano ya kimataifa.
Ikumbukwe kwamba kilio kikubwa cha Palestina ni kuonewa
pamoja na kuporwa haki zao asilia (ardhi) hivyo kubaki kama watoto yatima.
Pengine ni kwa kutambua ugumu wa mgogoro huo ndiyo maana Rais
wa Marekani, Donald Trump alisema:
“Uongozi wangu unaunga mkono uundwaji wa taifa moja ili
kumaliza mzozo wa Israel na Palestina,”.
Anachosema Trump nacho ni tatizo kwa sababu ni nani kati ya
Palestina na Israel atakubaliana na hilo?
Ukimsikiliza Netanyahu ni kana kwamba anataka Israel imiliki eneo
lote linalokaliwa na Palestina.
Tusisahau kuwa hivi sasa Israel inafikiria kuanzisha makazi
mapya 6000 ingawa haifamiki yatatoka eneo la Palestina au la.
Huu ni mgogoro mwingine kama nilivyogusia katika mada
iliyopita. Hii inaonesha hali bado si shwari.
Kama hiyo haitoshi, Waziri Mkuu wa Israel alimwambia Trump
lazima Wapalestina waitambue Israel kama taifa la Kiyahudi na kutambua haki ya
Israel kusimamia usalama katika eneo zima.
Hata hivyo, Trump alionekana kutomuunga mkono Netanyahu
kuhusu suala hilo hususan eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa lugha nyingine Trump amevunja utamaduni wa viongozi wa
Marekani kuikumbatia Israel. Hii inaashiria nini?
Tuseme kwamba ile dhana kuwa ukimuona Mwisrael umemuona
Mmarekani na ukimuona Mmarekani umemuona Mwisrael inafutika?
Pengine tukubaliane tu na ushauri wa Rais Trump kuwa pande
zote mbili zinahitaji kuwa na maridhiano.
Ni kwa njia hiyo pekee amani ya kweli itapatikana kati ya
Wapalestina na Waisrael na si vinginevyo.
Lakini viongozi wakitanguliza jazba na ubabe kama anavyotaka
Netanyahu badala ya amani ni vita.
SHARE
No comments:
Post a Comment