Kulingana na muswada wa pendekezo la bajeti ya shirika la ulinzi wa
mazingira la Marekani EPA, utawala wa rais Donald Trump utapunguza
programu zinazonuwia kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi na
kuboresha usalama wa maji na ubora wa hewa. Ufadhili wa shirika hilo
utapunguzwa kwa karibu asilimia 25 na karibu watu 3000 watapoteza ajira
zao. Shirika hilo la ulinzi wa mazingira EPA, linaongozwa kwa sasa na
Scott Pruitt, aliyehoji muafaka wa kisayansi kwamba shughuli za
kibinadamu zinachangia kuongezeka kwa joto la dunia. Trump anapanga
kuwasilisha bajeti yake kwa bungeni tarehe 13 mwezi Machi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment