Merkel kukutana na Trump Machi 14
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kukutana na rais wa
Marekani Donald Trump mjini Washington tarehe 14 mwezi huu wa Machi.
Taarifa za kina juu ya mkutano huo bado hazijatolewa, lakini utafanyika
baada ya Trump kuikosoa sera ya kiliberali ya Merkel kuhusu wakimbizi,
ambayo ilipelekea zaidi ya waomba hifadhi milioni moja kuingia nchini
Ujerumani tangu mwaka 2015. Merkel kwa upande mwingine, amekuwa
akimkosoa Trump, alimkumbusha juu ya maadili ya kidemokrasia wakati wa
mazungumzo yao kwa njia ya simu baada ya kuchaguliwa kwake mwaka
uliopita. Hii ndiyo itakuwa mara ya kwanza kwa kansela Merkel kukutana
na Trump akiwa rais.
No comments:
Post a Comment