Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katikahafla ya
uwekaji wa jiwe la msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho
kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.
Balozi
wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akizungumza katika hafla
yauwekaji wa jiwe msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho
kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.Picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kushirikiana na Balozi wa
China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing wakiweka jiwe la msingi kuanza
ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani
450,000,jana jijni Dar e Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiteta jambo na Balozi wa China
nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wananchi wakishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa
kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana
jijni Dar e Salaam.
Katibu
Tawala Manispaa ya Temeke, Hashim Komba akizungumza machache katika
hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa kiwanja cha
Bandari
Bila
shaka kila mmoja wetu anakumbuka ahadi ya RC Makonda aliyoitoa mwaka
jana ya kujenga viwanja vitatu (3) vya mpira kwa ajili ya maendeleo ya
mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo Ndondo Cup kwani mashindano
haya kwa ujumla wake yanalenga kuboresha mazingira ya michezo na
kuzalisha vipaji vingi zaidi ambavyo vinabeba ajira nyingi za vijana
ndani yake.
Kimsingi
RC Makonda hakuishia tu kuahidi bali alikwenda mbali zaidi na kumualika
balozi wa China kushuhudia hali halisi ya viwanja vinavyotumika kwa
sasa kama sehemu ushahidi wa kile alichokuwa amemueleza wakati
akimshawishi.
Ikiwa
imepita miezi kadhaa tangu Balozi kukubaliana na ombi la Mkuu wa Mkoa,
leo tarehe 3 Balozi huyo wa China akiwa na RC Makonda wameweka historia
mpya baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa viwanja hivyo,
huku wakianza na kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za
Kimarekani 450,000,
Huku
kikijengwa kwa viwango vya kimataifa na kampuni iliyojenga uwanja wetu
wa taifa. Kuonyesha na kutambua utendaji na msukumo mkubwa wa RC Makonda
katika kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto
za wanyonge, Balozi pia amemuahidi Mkuu wa Mkoa kutoa kipaumbele cha
ajira vijana wote watakaoshiriki mashindano ya Ndondo Cup kwenye kampuni
mbili ambao watakuwa vijana zaidi ya 20000.
SHARE
No comments:
Post a Comment