Timu
ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya
bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya wachambuzi wa
soka wamesema kuwa kutokana na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana
ikawa ndiyo nafasi kwa yanga kutetea ubingwa wao ambapo baada ya mchezo
wa leo Simba wamebaki na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita kileleni
wakiwa na pointi 56 baada ya michezo 25.
katika
mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba ulishuhudia timu ya soka
ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta
wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka
Yusuph Huku bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la
kufutia machozi kwa Simba sports Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika
61 ya kipindi cha pili.
Kwa
matokoe hayo yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na
jumla ya pointi 56 wakifuatiw ana Simba wenye pointi 55 huku Kagera
Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na
Azam wenye pointi 44.
Zacharia
Hans Poppe akiwa hana hamu baada ya kushuhudia Timu ya Simba ikinyukwa
bao 2-1 na Timu ya Wanankurukumbi Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kagera
Sugar leo hii jumapili.
Kikosi cha Simba kilichoanza
Kocha
mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haamini kilichotokea baada ya
timu yake kufungwa bao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu
bara uliopigwa uwnaja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kichuya Akiambaa na Mpira
Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude akitafakari baada ya timu yake kuchapwa bao 2-1 na Kagera Sugar.
Winga wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiambaa na mpira wakati mchezo ukiendelea
SHARE
No comments:
Post a Comment