Wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad
wakifurahia kuwasili kwa ndege yao ya 10 na ya Mwisho aina ya A380
Ndege ya Etihad A380s inatoa huduma kutokea nchi za
uarabuni kwenda mji mkuu wa London, Sydney, New York na kuanzia tarehe
01/07/2017 watakua Paris.
Wafanyakazi wa shirika la Ndege la Etihad wakijumuika
pamoja katika uwanja wa ndege wa Hamburg Finkenwerder nchini ujerumani barani
Ulaya ambapo ndege hiyo ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa shirika la ndege
la uarabuni kabla ya kuanza safari zake za uwasilishaji nchini Abu Dhabi.
Ndege za aina ya A380s zilizojishindia tuzo kadhaa, ni
ndege za kibiashara zenye utofauti wa kipekee kwenye huduma zao kama malazi
–vyumba vitatu vyenye ukubwa wa kuweza kuishi watu mpaka wawili vikiwa na
sebule, bafu binafsi na chumba cha kulalia. Ndege hizi pia zinajivunia kuwa na
“appartments” 9, studio za biashara 70, mahala pa kupumzikia na siti nzuri 415
kwenye daraja la uchumi.
SHARE
No comments:
Post a Comment