TRA

TRA

Thursday, May 25, 2017

CCM YAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA HARAKA JUU YA MAUAJI YANAYOENDELEA KIBITI, MKURANGA NA RUFIJI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


POLEP
Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.
          Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es salaam  jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea katika Wilaya hizo.
          POLEPOLE pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.
          Amesema chama kwa muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa imetosha.
Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema mauaji hayo yanakiweka Chama katika mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake hivyo ni vema hatua zikachukuliwa sasa.
          Katika hatua nyingine, POLEPOLE amesema Chama kimeipongeza Kamati Maalum ya kuchunguza Mchanga wa Madini kwa kazi nzuri iliyofanywa sanjari na kuwaomba wananchi kumuunga mkono Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua alizozichukua kwa watendaji kutokana na Ripoti ya Mchanga wa Madini.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger