Mchoraji
Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu akiwa katika Idara ya
Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
uchunguzi wa afya yake. Mzee Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea
Hospitali ya Amana.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara hiyo
Juma Mfinanga akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dar es salaam 25-05-2017
Hospitali
ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji wa Nembo
ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu .Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema Mzee Kanyasu amechukuliwa
leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani
zake na kupatiwa matibabu ya awali.‘’ Tumemchukua kutoka Hospitali ya
Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo vya habari kuwa hali
yake kiafya sio nzuri hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa
Lawrence Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili
‘’ Amesema Dk. Juma.’ Wenzetu wa Hospitali ya Amana wamemfanyia
uchunguzi wa awali na wakatueleza shida yake kubwa ni kukosa nguvu na
kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara ya magonjwa ya Dharura na
Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi tutamuanzishia
tiba haraka kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa MNH.’’ Amesema
Dk. Juma.
Kwa mujibu wa Dk. Juma kukosa lishe , mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa mbalimbali.
SHARE








No comments:
Post a Comment