Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dkt. Abdalla Juma Mabodi pamoja na viongozi wengine wakipeleka bati
kwa mafundi wanaoezeka msikiti wa ijitimahi.
Msafara uliofuatana na Naibu
katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “Mabodi”
wakionyeshwa maeneo mbali mbali ya Ijitimai hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja
Vuai Mwinyi Mohamed (kushoto) akimuonyesha Naibu katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “Mabodi” ramani ya msikiti na nyumba
zingine zinazotakiwa kujengwa katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja
Vuai Mwinyi Mohamed (kushoto) akimuonyesha Naibu katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “Mabodi” ramani ya msikiti na nyumba
zingine zinazotakiwa kujengwa katika eneo hilo.
Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dkt. Abdalla Juma Saadala “Mabodi” pamoja na viongozi wengi wakiomba
dua mara baada ya kufanya shughuli za ujenzi.
………………………………..
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
INAWEZA kuchukuliwa ni kama staili ya
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana anayofanya kwa sasa Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar,
Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” ya kuwa karibu na wana CCM na
wananchi visiwani Zanzibar, katika kuinua morali ya wana CCM kukipenda
chama chao na kushirikiana na wananchi katika shida na raha ambapo
Kinana alionyesha njia kwa yeye mwenyewe kushiriki kazi mbalimbali za
kijamii.
Kwa upande wake tangu ateuliwe kuwa
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Dkt. Abdallah Juma Saadallah
almaarufu kama "Mabodi" amekuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya
Visiwani Zanzibar kuimarisha chama na sasa yalipotokea mafuriko visiwani
humo ameelekeza nguvy zake katika kuwafariji waathirika na kushirikiana
nao katika kurejesha miundombinu yao binafsi kama nyumba katuka kufanya
ujenzi wa nyumba zilizoathirika na mafuriko ya mvua. Mei 14, Dkt.
"Mabodi" amewasihi viongozi na waumini wa
dini ya kiislamu kutumia fursa ya Ijitimai kuliombea taifa liendelee
kudumu katika hali ya Amani na Utulivu.
Nasaha hizo amezitoa mara baada ya
kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Msikiti wa Ijitimai ya
Kimataifa huko katika kijiji cha Kidoto Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema mamia ya waumini wa dini
ya kiislamu watakaoshiriki katika ijitimai hiyo watakuwa ni sehemu
muhimu ya kufanya dua mbali mbali za kuimbea nchini inusurike na maafa
ili wananchi waendelee na shughuli zao za kijamii.
Alieleza kwamba CCM inaunga
mkono juhudi zinazofanywa na taasisi za kidini nchini katika kuhubiri
amani na mshikamano kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla.
Alisema licha ya Chama hicho kuwa
ni taasisi ya kisiasa bado kina jukumu kubwa la kushiriki kikamilifu
katika shughuli za kidini zinazoendeshwa na wananchi wa wa itikadi
tofauti za kisiasa.
Aidha kwamba Chama Cha Mapinduzi
Zanzibar kitatoa msaada wa kupeleka nguzo za umeme katika nyumba ya
wageni pamoja na kununua vifaa vya samani za ofisi ya jumuiya
inayosimamia Ijitimai hiyo ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Akitoa taarifa juu ya maendeleo ya
Ijitimai hiyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Mwalim Hafidh amesema
bado wanaendelea kumalizia ujenzi wa msikiti utakaochukua waumini zaidi
ya 5100 kwa wakati mmoja.
Alisema bado wanakabiliwa na
changamoto za upungufu wa vifaa vya ujenzi wa mabanda yatakayotumika
wakati wa Ijitimai pamoja na ujenzi wa shule , chuo cha madrasa,
hospitali na maktaba pamoja na miundombinu mingine nyingine ya kijamii.
Aidha ameupongeza uongozi wa CCM
kwa ziara hiyo na kueleza kuwa taasisi nyingi za kisiasa zimekuwa
hazishiriki ipasavyo katika masuala ya kidini hali inayosababisha
kutokuwepo na ushirikiano mzuri kwa taasisi hizo.
Naye Makamo Mwenyekiti wa
Jukumiya Fiysabilillah Tabligh Markaz Zanzibar, Sheikh Wakat Hassan
Bakar Alisema lengo la jumuiya hiyo ni kukifanya kijiji hicho kuwa
chimbuko la uislamu na ibada.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameambatana
na baadhi ya ujumbe kutoka Baraza la Wazee CCM Zanzibar, Uongozi
wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkuu wa Mkoa huo, Vuai Mwinyi
Mohamed.
Ijitimai hiyo inatarajiwa
kufanyika Mai 19, mwaka huu na kuudhuriwa na wageni kutoka nchi za
Kenya, Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda, Ethiopia na Jamhuri ya
kidemokrasia ya Kongo.
SHARE
No comments:
Post a Comment