Timu ya Everton ya England yenye
wachezaji nyota akiwemo Mbelgiji, Romelu Lukaku, itazuru Tanzania
kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya wa 2017/18, tovuti ya klabu
hiyo imeandika.
Ziara hiyo ambayo itakuwa sehemu ya sherehe zao za udhamini
mpya wa kampuni ya SportPesa, itaifikisha The Blues kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam unaomeza mashabiki 60,000 kucheza mechi Alhamisi ya
Julai 13.
Everton itakuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England daima
kucheza mechi ukanda wa Afrika Mashariki – na itamenyana na bingwa wa
mashindano ya SportPesa Super Cup.
Nchi mbili, Tanzania na Kenya
zitakutanisha timu zao nane, nne kutoka kila upande katika michuano
hiyo, kuwania nafasi ya kucheza na kikosi cha Ronald Koeman.
Mapema mwezi huu, Everton ilitangaza udhamini mnono wa rekodi
na SportPesa wa miaka mitano na baada ya hapo kampuni hiyo ikaingia
Afrika Mashariki kufunga ndoa na klabu kadhaa kubwa, zikiwemo SImba na
Yanga.
Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza Juni 5 hadi
11 mjini Dar es Salaam, ikishirikisha timu za Simba SC, Yanga SC,
Singida United na Jang’ombe Boys za Tanzania, Gor Mahia, AFC Leopards,
Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya.
Bingwa wa michuano hiyo itakayofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam ndiye atamenyana na Everton.
SHARE
No comments:
Post a Comment