Hifadhi
ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro ni moja ya mbuga za wanyama ambazo kwa
sasa hujivunia idadi kubwa ya wageni na wanyama makundi tofauti wakiwemo
simba pia ni hifadhi ambayo hufikika kwa urahisi na kuwafanya wageni
kuona wanyama kwa haraka.
Hifadhi
imeshirikiana na vijiji katika kuunda ujirani mwema kupitia miradi
mbalimbali ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi ili kuhakikisha maafisa
wa wanyamapori wanashirikiana na wanavijiji kulinda mipaka ya hifadhi
ya taifa mikumi dhidi ya ujangili.
Mbuga
ya wanyama Mikumi hupokea wageni wa aina mabalimbali wakimiwemo wenyeji
wakazi kwa vingilio tofauti ukilinganisha na watalii wandani ambapo
vingilio vyao ni shilling 5700 kwa mtu mzima.
Muongozaji
wa hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa mkoani Morogoro Yuston Bonike
akimuonyesha muandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Ashton
Baraigwa mbegu ya mimea ambayo inaweza kuliwa na nyani kipindi cha
ukosefu wa chakula na kumletea madhara na nyani huyo kugeuka kuwa
kichaa.
Moja
wa maporomoko ya maji kivutio ambacho kina patikana katika hifadhi ya
taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambacho hufikiwa kirahisi
kwa njia ya miguu na hupatikana ndani ya msitu huo.
Moja ya mnyama anayepatikana katika hifadhi hiyo anayejulikana kwa jina maarufu “digidigi” akiwa ndani ya Msitu huo
Hali halisi ya mazingira ya hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambapo ofisi zake hupatika hapo mbele
Mafundi
wakiwa katika ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Lumango Wilayani
Kilosa mkoani Morogoro mradi wa ujirani mwema unaotekelezwa na Hifadhi
ya taifa mikumi kwa asilimia 70 huku wananchi wakichangia nguvu kazi
kwa asilimia 30. Nia na madhumuni ya ushirikiano huo ni kulinda na
kuhifadhi mipaka ya TANAPA pamoja na kutoa taarifa za ujangili.
Moja
ya jengo la Zahanati ambalo limeanza kutumika katika Kijiji cha Ihombo
kata ya Mikumi mkoani Morogoro ambayo hupokea wagonjwa wasiopungua 300
kwa mwezi mradi ambao ulitekelezwa na Hifadhi ya taifa Mikumi kwa lengo
la kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema na ulinzi wa mipaka ya
hifadhi hiyo.
Tembo
nao ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi ya
taifa Mikumi mkoani Morogoro ambao mara nyigi hupenda kutembea kwa
makundi wakati wa kujitafutia malisho.
Kikundi
cha utunzaji wa mazingira kinachotokana na mradi wa utalii wa
kitamaduni wakiwa wameshikilia vikapu ambavyo vimetengenezwa na
mifuniko ya chupa za maji ambayo wamekuwa wakiyaokota. Wa pili kutoka
kulia ni katibu wa kikundi hicho Bw. Christandus Mdoe.
Wageni
wa kitalii katika hifadhi ya taifa mikumi mkoani Morogoro
wakijadiliana kitu nje ya ofisi ya mapokezi huku wakifurahia mazingira
ya eneo hilo la wanyama wakionyesha jinsi walivyo na amani katika eneo
hilo.
Silas
Bakari fundi ujenzi wa nyumba za kitamaduni akionyesha matumizi ya
vyumba katika maeneo ambayo yamejengwa na chupa ambazo huokotwa
kandokando ya hifadhi ya taifa mikumi na maeneo mengine, jinsi
ambavyo chupa hizo zitakavyoboreshwa na kuifanya nyumba kuwa kivutio
ch a utalii wa kitamaduni kwa wageni.
SHARE
No comments:
Post a Comment