TRA

TRA

Monday, May 15, 2017

HIKI NDIYO SABABU YA LWANDAMINA KUTAKA NGOMA ASIONDOKE YANGA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amemuorosha mshambulizi Donaldo Ngoma katika idadi ya washambulizi anaowataka msimu ujao.


Hali hiyo imeonekana kuwashangaza baadhi kwa kuwa wanaamini Ngoma ataondoka na tayari mapenzi ya Wanayanga yameanza kuondoka kwake.


Mkataba wa Ngoma umebakiza mwezi mmoja tu kuisha na uongozi wa Yanga ulitangaza kwamba mchezaji anayetaka kuondoka ruksa na kumekuwa na taarifa kuwa Ngoma yuko kwenye rada za watani wao Simba.


Taraifa za ndani kutoka Yanga, zimeeleza, Lwandamina anataka mshambulizi mwenye usumbufu kama wa Ngoma kwa kuwa anakuwa anwachosha mabeki kama ilivyo kwa Jesse Were raia wa Kenya ambaye anakipiga Zesco ya Zambia aliyokuwa anaifundisha kabla ya kutua Yanga.


"Unaona Chirwa anaanza kuimarika, ni msumbufu lakini anatokea pembeni. Kocha angependa kupata mchezaji msumbufu pia katikati ya uwanja.


"Anaamini hiyo itampa nafasi ya mchezaji kama Tambwe kufunga kwa urahisi. Naamini wamezungumza na Ngoma," kilieleza chanzo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger