MBUNGE wa Singida Kaskazini, Mhe.Lazaro
Nyalandu amesema Ubalozi wa Marekani umetoa hati ya kusafiria (visa) kwa ajili
ya kuwawezesha wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vincent kupata matibabu
nchini Marekani.
Katika ukurasa wake wa Facebook leo Nyalandu
amesema waliopata Visa ni wazazi,watoto na wataalamu wawili wa afya ambao
watasafiri kwenda Marekani.
"Wote wamepewa visa asubuhi ya leo
Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam. Akina Mama watatu, watoto wote watatu, na
Daktari Moja na Nurse Moja. Kansela wa Ubalozi wa Marekani alinipigia simu
asubuhi akiwasubiri katika siku ambayo haikuwa ya kazi,” amesema Nyalandu na
kuongeza:
“Mungu ambariki sana kwa moyo huu. Napenda pia
kutoa taarifa kuwa ndege yao aina ya DC 8 inatarajiwa kutua Leo usiku saa 2:15
majira ya Afrika Mashariki katika uwanja wa KIA. Mungu wa Watanzania awabariki
wote kwa sala na dua zenu kwa ajili ya hawa watoto. Sifa na utukufu kwa Mungu
wetu.”
Katika taarifa ya awali kwa vyombo vya habari
Nyalandu amesema safari ya kuelekea Marekani itakua kesho asubuhi na ndege
itatua Charlotte,New York na kisha wagonjwa pamoja na waliowasindikiza
wataingia katika ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa hadi katika mji wa
Sioux City,Iowa
Watoto hao watatu walijeruhiwa wakati wakiwa
katika safari ya masomo wilayani Karatu mkoa wa Arusha jumamosi iliyopita na
kusababisha vifo vya wanafunzi 32,walimu wawili na dereva wao.
SHARE
No comments:
Post a Comment