Mchezaji wa Shule ya Sekondary
Chang’ombe, Hamad Hemed (kulia), akiwania mpira na mchezaji wa Shule ya
Makongo, Muksin Mohamed, wakati wa michuano ya Copa/UMISSETA
yaliodhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola, kwenye Uwanja wa Taifa Dar Es
Salaam
Mchezaji wa Shule ya Sekondari
Makongo (kushoto), akiwania mpira na mchezaji wa Shule ya Chang’ombe
Tarik Hassan, wakati wa michuano ya Copa/UMISSETA yaliodhaminiwa na
Kampuni ya Coca-Cola, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akikagua timu za Sekondary
zilizoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson
Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa timu za Sekondari
zilizoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa
kampuni ya Coca-Cola Bw. Eric Ongara akiongea machache wakati wa
ufunguzi wa michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za
Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akifungua michezo ya Copa/UMISSETA
ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni
mwa wiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akigawa vifaa vya michezo kwa shule
za sekondari zinazoshiriki michezo ya Copa/UMISSETA.
Dhana ya kuwekeza katika sekta ya
michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari imekua ikileta manufaa
makubwa kwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao wamekua
wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya chini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua
akifungua michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za
Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahishwa na juhudi
zinazofanywa na kampuni ya Coca-Cola katika kuhakikisha tunaimarisha
sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo
tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa kupata wanamichezo mahiri wa
baadaye” amesema Waziri Mwakyembe.
Aidha aliongeza kuwa Serikali
itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja
na kuchangia katika uchumi wa nchi. Vilevile aliwataka walimu kufuata
ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha michezo mashuleni ikiwemo
kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio kuvitumia vipindi hivyo
kwa shughuli nyingine.
Mhe. Mwakyembe aliwataka wazazi
na walezi kuhakikisha kuwa wanawapatia watoto wao nafasi ya kucheza na
kujifunza michezo mbalimbali inayowajenga kimwili na kiakili.“Michezo
inafaida kubwa kwa afya ya binadamu ikiwemo kuimarisha akili na mwili,
kujenga ushirikiano na urafiki baina ya watu “ alisema Mhe. Mwakyembe.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali
watu wa kampuni ya Coca-Cola Bw. Eric Ongara alisema kuwa kampuni ya
Coca-Cola inaamini katika kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini ndio
maana wamekua wakidhamini mashindano hayo.
Pia aliongeza kuwa kampuni ya
Coca-Cola itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa
michezo inazaa matunda na kufikia lengo lililokusudiwa la kuibua vipaji
vya michezo na kuviendeleza.
Michezo ya COPA UMISSETA
ilifunguliwa rasmi Mjini Dodoma Aprili 28 mwaka huu ambapo kitaifa
yanatarajiwa kuanza Juni 6 hadi 15 mwaka huu katika Viwanja vya Chuo cha
Ualimu Butimba Jijini Mwanza.
SHARE
No comments:
Post a Comment