Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo katika Kijiji cha Masakta, Bibi Magreth Mgeni (kushoto) wakikagua mahindi katika moja ya mashamba waliyoyatembelea. |
Katibu wa Homari AMCOS, Bw. Abdul
Msangi (kulia) akiwakaribisha wageni Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania walipotembea AMCOS hiyo.
Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo
katika Kijiji cha Masakta, Bibi Magreth Mgeni (kushoto) akizungumza na
wageni kutoka TADB walipotembea AMCOS hiyo. Wanaomsikiliza ni Mwenyekiti
wa RIVACO, Bw. Lohay Langai (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya
Homari AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa
Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo
wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akitaja fursa za mikopo
inayotolewa na Benki ya Kilimo wakati wa kikao cha pamoja kati ya TADB
na Bodi ya Homari AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya
mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
Sehemu ya mahindi yaliyokwisha vunwa yakiwa yamehifadhiwa Kijijini Masakta.
Mwenyekiti wa Gendi AMCOS, Bw.
Petro Dali (aliyesimama) akizungumza wakati wa mazungumzo na TADB
(hawapo pichani). Bw. Dali alizungumzia umuhimu wa Sekta ya Kilimo na
mchango wa TADB katika sekta hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (aliyesimama kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi
ya Gendi AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa
Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
Mwenyekiti wa Gallapo AMCOS, Bw.
Orondi Doita (aliyesimama) akizungumza wakati wa mazungumzo na Benki ya
Kilimo (hawapo pichani). Bw. Doita alitoa wito kwa Benki ya Kilimo
kuanza kuwakopesha ili waweze kujipanga mapema katika ununuzi wa mazao
kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya
Gallapo AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa
Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
…………………………………
Na Mwandishi wetu, Manyara
Katika kufanikisha azma yake ya
kuwa benki kiongozi katika kuleta maendeleo ya kilimo nchini Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imevitembelea vya ushirika vya
msingi mkoani Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
Akizungumza wakati wa ziara zake
katika vijiji vya Masakta, Gallapo na Gendi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki yake ina Dira ya kuwa
benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na
uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Hivyo
TADB ina wajibu wa kuwasaidia wakulima nchini ili kuwafikisha katika
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Bw. Assenga aliongeza kuwa kwa
kutambua umuhimu wa kuwanyanyua wakulima katika uongezaji tija wa kilimo
nchini kwa kutoa mikopo na kusaidia shughuli mbali mbali za uongezaji
tija katika kilimo.
“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima
TADB kwa kushirikisha wadau wa Kilimo, utafiti na huduma za ugani
tumejipanga kuwapatia wakulima mafunzo ya kilimo cha kisasa cha ili
waweze kutumia mbinu bora za kilimo,” alisema.
Akizungumza katika kikao chao na
ugeni wa TADB, Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo katika Kijiji cha
Masakta, Bibi Magreth Mgeni alisema kuwa TADB imekuja wakati muafaka kwa
kuwa itachagiza juhudi za kuinua na ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini nchini Tanzania.
“Kwa kweli tunapongeza kwa
kuanzishwa Benki hii kwa kuwa kwa miaka mingi mikopo mingi kutoka
taasisi za fedha imekuwa ikielekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za
bidhaa na kuwa na riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo,” alisema.
Naye Bw. Petro Dali, ambaye ni
Mwenyekiti wa Gendi AMCOS alipongeza uanzishwaji wa TADB kwa kuwa licha
ya umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo hasa kwa
wakulima wadogo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kuu ikiwa
ni ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo
ya kilimo nchini.
“Benki imekuja wakati muafaka kwa
kuwa tunaamini itatusaidia katika kupata mikopo nafuu ya ununuzi wa
pembejeo za kilimo na gharama na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza
tija katika kilimo,” alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Gallapo AMCOS, Bw. Orondi Doita alitoa wito kwa Benki ya Kilimo kuanza
kuwakopesha ili waweze kujipanga mapema katika ununuzi wa mazao ili
waweze kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha chakula kinabaki nchini
ili kuongeza usalam wa chakula.
Kuanza kufanya kazi kwa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kunaleta suluhisho la changamoto
nyingi zilizokuwa zinaikabili sekta kilimo nchini kwani inalenga
kuboresha upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwenye miradi ya
maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya viwango vya
kibiashara kwenye soko.
SHARE
No comments:
Post a Comment