Kundi la waandishi kumi wa habari kutoka nchini Israel wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Gombe hivi karibuni kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). (Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii).
Mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe, Elihuruma Wilson (kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa kundi la wanahabari kumi kutoka nchini Israel walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA).. (Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii).
Kundi la waandishi kumi wa habari kutoka nchini Israel wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma katika ziara yao ya hivi karibuni kutembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). (Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii).
Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (wa pili kulia) akionesha kifaa maalum cha kupigia picha za angani (drone) kilichorushwa na mmoja wa mwanahabari wa Israel walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). (Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii).
Wanahabari wa Israel wakipiga picha Sokwe wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). (Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii).
Na Hamza Temba, Kigoma
Kundi la wanahabari kumi
akiwemo muigizaji mmoja na maofisa wa kampuni ya utalii ya Safari kutoka nchini
Israel limetembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma na kufurahia
vivutio lukuki vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo na kuahidi
kuvitangaza watakaporudi nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na
Utalii kupitia TANAPA na Bodi ya Utalii kutangaza vivutio hivyo nchini humo.
Akizungumza hivi karibuni mara
baada ya kukamilika kwa ziara hiyo ya siku mbili, Kiongozi wa kundi hilo, Ronit
Hershkovitz alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wamefurahia
kuona vivutio vya kipekee katika hifadhi hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri
wa vivutio hivyo nchini Israel.
“Ni furaha kubwa kuwa hapa
Gombe, tumeona makundi ya Sokwe na fukwe nzuri za Ziwa Tanganyika, tuko hapa
kwa ajili ya kwenda kueleza kivutio hiki na vivutio vingine vya Tanzania nchini
Israel, Waisrael wanaipenda Tanzania na wanapenda kutembelea Tanzania, tumeona
ongezeko kubwa la watalii katika miaka ya hivi karibuni kutoka Israel baada ya
kazi ngumu ya muda mrefu, sasa tuna furaha kuona watalii wengi wanaongezeka na
tungependa kuona pia Watanzania wengi wakitembelea Israel,” Alisema Ronit.
Aliongeza kuwa, “Tunaenda
kueleza taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii, magazeti, televisheni na
popote tutakapoweza, lakini kubwa zaidi ni kuwaeleza marafiki zetu ana kwa ana
uzuri wa Tanzania kwasababu tunaipenda Tanzania, nakupenda sana”.
Walfson Noa, ambaye ni
Mwandishi wa Mitandao ya Kijamii na Meneja Masoko wa Kampuni ya Utalii ya
Safari ya Israel alisema, “Tulifanya matembezi kuwaona Sokwe wanaovutia sana huku
wakiishi katika mazingira yao ya asili, hili ziwa ni la maajabu sana (Ziwa
Tanganyika), hata nyani nao walikuwa wakijaribu kuingia kwenye mahema yetu ni
jambo la kuvutia, katika mtizamo wa kimasoko hili ni eneo ambalo nitawashauri
wateja wangu watembelee, ni kitu ambacho watu wanatakiwa kukifahamu, kugundua
siri ya uzuri wa hifadhi ya Taifa ya Gombe”
Kwa upande wake Meneja wa
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete ambaye
alikuwa kiongozi wa msafara huo akishirikiana na Meneja Mawasiliano TTB,
Geofrey Tengeneza, Meneja Mawasiliano wa TFS, Glory Mziray na Afisa Mawasiliano
wa Wizara ya Maliasili, Hamza Temba alisema ujio wa wanahabari hao utaleta
chachu ya kuongezeka kwa watalii wengi kutoka Israel pamoja na kupanua soko la
utalii kwa hifadhi za mikoa ya magharibi mwa Tanzania ikiwemo hifadhi ya Gombe.
“Tumekuja na kundi hili la wanahabari
ambao wameamua kama mlivowasikia kwa dhati kabisa kwamba watakaporudi nyumbani
watatumia mitandao ya kijamii, radio mbalimbali, Televisheni lakini kubwa zaidi
magazeti, wataandaa makala na vipindi mbalimbali hivyo tunaamini kwa dhati
kabisa watakaporudi nyumbani na kuzifanyia kazi taarifa zote walizozipata
katika hifadhi ya Taifa ya Gombe ama kwa hakika tutashuhudia ongezeko kubwa la
watalii kutoka nchini Israel katika siku chache zijazo,” Alisema Shelutete.
Aliongeza kuwa, “Ni wajibu
wa kila Mtanzania kuhakikisha rasilimali hizi za hifadhi zinazopatikana katika
hifadhi za taifa zinaendelea kutunzwa kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi
vijavyo, watalii hawaji kuangalia ng’ombe kwenye hifadhi zetu, nasisitiza kuwa mifugo
haikubaliki kwenye hifadhi zetu”.
Msafara huo ulikuwa na
wanahabari kutoka vyombo maarufu nchini humo ikiwemo kituo cha Televisheni cha Channel
2, Jarida la Atmosphere, Jarida la National Geographic, Jaria la wiki la Yediot
Acharanot -7 Yamim na waandishi wawili wa mitandao ya kijamii. Wengine ni
maofisa wawili wa kampuni ya Utalii ya Safari ya nchini humo.
SHARE
No comments:
Post a Comment