TRA

TRA

Monday, May 8, 2017

Emmanuel Macron ashinda uchaguzi wa urais Ufaransa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 
Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa wafaransa waliompa.


 Macron ndiye rais wa umri mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa Ufaransa 


"Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu vya kidemokrasia, na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa," amesema.




Macron anasema ni heshima kubwa na mmenipa wajibu mkubwa wa kutekeleza, bila kauli yoyote kwangu, natoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu.

 
  Wafuasi wa Macron wakisherehekea eneo la Louvre mjini Paris 
 
"Shukrani hizi zimfikie kila mmoja wenu, kwa kura yako na kuniunga mkono. Sitasahau kamwe, nitakuwa muangalifu sana na nitahakikisha kwa nguvu zangu zote naheshimu imani yenu kwangu."
Le Pen amempongeza Macron kwa njia ya simu na kusema kwamba chama chake cha National Front kimepata ushindi mkubwa kwa kugawana kura, na kufanikiwa kuigawa Ufaransa kati ya wazalendo na watawala.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa Macron wakisherehekea eneo la Louvre mjini Paris
Marine Le Pen aliyekuwa na matumaini ya kuikwaa nafasi ya rais wa Ufaransa tayari amekubali kushindwa dhidi ya mpinzani wake Emmanuel Macron.


      Wafuasi wa Macron wakisherehekea nje ya Louvre, Paris

"Watu wa Ufaransa wamemchagua rais wa Jamhuri, na wameamua kuwa na muendelezo. Nimempigia simu bwana Macron kumpongeza kutokana na ushindi wake kwasababu nina wiwa moyoni mwangu na ninaitakia mema nchi hii.
"Nimemtakia mafanikio mema katika changamoto zinazoikabili Ufaransa. Ningependa kuwashukuru raia wa Ufaransa milioni kumi na mmoja, ambao waliamua kunipa mimi sauti zao na imani yao juu yangu, pamoja na wanaharakati, ambao waliniunga mkono na kunipa ushirikiano wakati wote wa kampeni.


Uchaguzi wa urais Ufaransa una maana gani kwa Afrika
Bw Macron alisema ushindi wake ni ushindi wa bara Ulaya.
"Nina furaha kubwa, kwa sababu ni ushindi mkubwa kwa Ulaya yote, ni ushindi kwa ulaya, ni mkubwa. Wafaransa walionesha furaha yao.
"Ushindi mkubwa wa asilimia sitini na tano, hatukulitarajia hilo, na, ndio hivyo, ni utawala mwingine kwa Ufaransa. Huwezi kuamini, nina matumaini kwamba naamini atapata uungwaji mkono katika uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Juni na huenda ukaleta mabadiliko makubwa nchini. Itastaajabisha."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wafuasi wa Macron wakisherehekea nje ya Louvre, Paris
Le Pen naye alisikika akisema: "Nimeridhika sana, ushindi huu umeiokoa Ulaya, nastaajabia kabisa, ni suala halisi, naamini itasababisha Ulaya ijichekeche, nafikiri italeta mabadiliko makubwa, tutashuhudia mabadiliko makubwa yakiambatana na maelekezo mapya, ni ajabu, mastaajabu, asante."

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger