Polisi nchini
Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London
hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la
Jumamosi ambapo watu saba waliuawa na wengine wapatao hamsini
walijeruhiwa.
Watu kumi na mmoja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London.
Kundi la Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo.
Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio la London ametajwa katika vyombo vya habari.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasio kuwa na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake.
Watu 21 waliojeruhiwa katika shambulio hilo wako katika hali mahututi.
SHARE
No comments:
Post a Comment