Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Waziri
Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika
kwenye viwanja vya Majengo Manispaa ya Mosjhi mkoani Kilimanjaro Juni 5, 2017 ambapo mwanasiasa wa upinzani, mbunge mstaafu wa CHADEMA na
Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, marehemu mzee Philemon
Ndesamburo (82), maarufu kama "Ndesa pesa" aliagwa. Maelfu ya watu
walijipanga kwenye barabara za Manispaa hiyo, wakati gari lililobeba
jeneza la mwili wa hayati Ndesamburo aliyefariki ghafla wiki
iliyopita.Mrehemu Ndesamburo atazikwa nyumbani kwake eneo la KDC
Kiborloni majira ya saa 7 mchana.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili
atika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Wabunge
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza
lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro,
Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Viongozi
mbalimbali wa Kisiasa na dini wakiwa wamesimama mara baada ya mwili wa
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon
Ndesamburo kuwasili uwanjani hapo
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye uzuni mara
baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro,
Phillemon Ndesamburo ulipokuwa unaelekea katika viwanja vya Majengo kwa
ajili ya kuagwa mwili huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment