Mwili
wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu umeagwa leo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao
Igokero wilayani Misungwi.
Shughuli
ya kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,
Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye
amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulusubisya.
Akizungumza
katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia
kwa kipindi alichokuwa amelazwa hospitalini hapo.
“Nawapongeza
Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu,
lakini kazi ya Mungu haina makosa , pia sina budi kuwashukuru majirani
zake na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye
hivyo hata kwa wazee wengine’’ amesema Katemba.
Naye
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga
amesema walimpokea Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana
alikokua akipatiwa matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali
waligundua kwamba ana maradhI ya Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa
muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua akiishi.
Hivyo
Dk. Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini
mapema pindi mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi
hospitali ni rahisi kupata tiba na kupona kuliko kusubiri hadi ugonjwa
uwe sugu.
Mzee
Francis Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017
saa mbili na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi
ya wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto wakiaga mwili wa marehemu Francis Maige Kanyasu (86) katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Marehemu alikuwa amelazwa katika
hospitali hiyo na wakati akiendelea na matibabu mauti yakamkuta.
Mwili
wa marehemu ukiwa umebebwa tayari kwa safari ya kuelekea Misungwi
mkoani Mwanza ambako mazishi yatafanyika.
0003: Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili wakisubiri kuuaga mwili huo
leo. Kulia ni Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi,
Agness Mtawa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk
Mpoki Ulusubisya akizungumza kabla ya shughuli za kuaga mwili huo leo.
Baadhi ya watu waliofika kuaga mwili huo leo.
Mkurugenzi wa Huduma na Upasuaji wa Muhimbili, Dk Julieth Magandi akiwashukuru watu mbalimbali walofika kuuaga mwili huo leo.
Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga
akieleza jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu
mzee Francis Maige Kanyasu.
SHARE
No comments:
Post a Comment