• About
  • Services
  • Products
  • Blog
  • Contact Us

NCHI YANGU

Menu
  • Home
  • Lifestyle
    • Sub Menu 1
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Sports
    • Sub Menu 1
      • Sub Menu 1
      • Sub Menu 2
      • Sub Menu 3
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Post
  • Fitness
  • Music
  • Travel
  • Politics
  • Beauty

TRA

TRA

Saturday, June 3, 2017

Home > > UEFA: Bingwa kati ya Juventus v Real Madrid kufahamika leo

UEFA: Bingwa kati ya Juventus v Real Madrid kufahamika leo

at 4:02 AM
Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane anakabiliwa na kizungumkuti cha kuamua nani kati ya Gareth Bale na Isco atacheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya leo.

Bale hajacheza tangu 23 Aprili lakini sasa yuko sawa kucheza.
Isco, ambaye alijaza pengo lake naye amekuwa akicheza vyema sana na amefunga mabao matano katika mechi nane walizocheza hivi karibuni.

"Wote wawili ni wachezaji muhimu sana na kila mmoja anaweza kutoa maoni yake lakini hilo halitaniathiri," Zidane amesema.
Mkufunzi wa Juventus Max Allegri wachezaji wake wote pia wako sawa kucheza.

Gianluigi Buffon, Giorgio Chellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic na Leonardo Bonucci walipumzishwa mechi ya mwisho ya Juve katika Serie A dhidi ya Bologna Jumamosi iliyopita.

Gianluigi Buffon, 39, atakuwa nahodha wa Juve katika mechi hiyo itakayochezewa Cardiff.
  • Borussia Dortmund na Legia Warsaw wavunja rekodi
Buffon hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
"Itakuwa na maana kubwa sana kwangu," anasema mchezaji huyo, ambaye amechezea Italia mechi 168.

 Bale na Isco wakitaniana wakati wa mazoezi, mmoja wao huenda atakosa nafasi ya kucheza

"Itakuwa siku ya furaha zaidi kwangu katika maisha yangu ya uchezaji, pamoja na Kombe la Dunia - kwa sababu itakuwa ni kama zawadi, baada ya safari ngumu yenye dhiki na visiki na bidii."
Juventus walilaza Monaco 4-1 na kufika fainali kwa mara ya pili katika misimu mitatu.
Real Madrid nao waliwatoa Atletico kwa ushindi wa jumla wa 4-2.
Ronaldo, ambaye alifunga penalti ya ushindi fainali msimu uliopita, anasema amepumzika vya kutosha na ako makini kabisa.
"Mwisho wa msimu ni muhimu sana," anasema.
Ronaldo alifikia magoli 400 ambayo amefungia Real msimu wa sasa, pamoja na mabao 100 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Haki miliki ya picha PA
Image caption Usalama utaimarishwa kwa ajili ya fainali
Hii itakuwa mechi ya 19 kwa klabu hizo mbili kukutana, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya.
Klabu hizo ndizo zilizokutana mara nyingi kabisa historia ya michuano hiyo, baada ya Bayern dhidi ya Real Madrid (24).
Juventus na Real Madrid, kila mmoja ameshinda mechi nane kati ya hizo, mechi mbili zikimalizika kwa sare.
Mechi yao pekee kukutana fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Real walishinda 1-0 mwaka 1998 kupitia bao la Pedrag Mijatovic.
Juventus wameshinda mara mbili pekee kati ya fainali nane walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya. Walishindwa fainali nne walizocheza karibuni zaidi mwaka 1997, 1998, 2003 na 2015.
Real Madrid wanapigania kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya misimu miwili mfululizo.
Mwaka huu ni mara ya tatu kwa Real Madrid kufika fainali katika misimu minne.
Juve ndiyo klabu pekee ambayo haijashindwa mechi yoyote msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, klabu ya kwanza tangu Atletico Madrid mwaka 2013/14 kufika fainali bila kushindwa.
Real Madrid nao wamefunga kila mechi kati ya mechi 12 walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu.
Unknown

Author: Unknown

SHARE
  • Share
  • Tweet
  • Share
  • Pin
  • Share
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Fourni par Blogger CodeEnvoyer par emailBlogThis !Partager sur TwitterPartager sur FacebookPartager sur LinkedInÉpingler sur PinterestPartager sur StumbleUponVoter pour cet article sur HelloCoton

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Tupate kupitia Facebook

Popular Posts

  • KWELI WANANCHI WANA SHIDA NYINGI, WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI
        ZAIDI ya Wananchi 3,000 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Januari 29, 2018 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar...
  • SINGIDA UNITED YAIBOMOA KAIZER CHIEF, YAMTWAA MSHAMBULIAJI HATARI KUTOKA ZIMBABWE
    Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakibad...
  • WANAFUNZI 106 SHULE YA MILAMBO TABORA WAKAMATWA
      Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi 106 wa shule ya Sekondari ya Milambo kwa madai ya kufanya vur...

Popular Posts

  • KWELI WANANCHI WANA SHIDA NYINGI, WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI
    KWELI WANANCHI WANA SHIDA NYINGI, WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI
        ZAIDI ya Wananchi 3,000 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Januari 29, 2018 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar...
  • SINGIDA UNITED YAIBOMOA KAIZER CHIEF, YAMTWAA MSHAMBULIAJI HATARI KUTOKA ZIMBABWE
    SINGIDA UNITED YAIBOMOA KAIZER CHIEF, YAMTWAA MSHAMBULIAJI HATARI KUTOKA ZIMBABWE
    Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakibad...
  • WANAFUNZI 106 SHULE YA MILAMBO TABORA WAKAMATWA
    WANAFUNZI 106 SHULE YA MILAMBO TABORA WAKAMATWA
      Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi 106 wa shule ya Sekondari ya Milambo kwa madai ya kufanya vur...
  • SBL yazindua bomba la 470m/- kudhibiti majitaka
    SBL yazindua bomba la 470m/- kudhibiti majitaka
    Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni y...
  • Dkt. Jakaya Kikwete ampongeza Samatta kwa kuibuka mshindi
    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea ...
  • MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WAIPIGA JEKI ZAHANATI YA MWINGIRO GEITA
    MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WAIPIGA JEKI ZAHANATI YA MWINGIRO GEITA
    Maafisa wa kitengo cha  Mahusiano ya Jamii katikamgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, William Chungu (kulia) na Zuwena Senkondo (kusho...

Pages

  • Home
  • About Us
  • Contat Us
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger