NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya
zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi
karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa
kustaafu kwa amani.
Katika
semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT
Capri-point jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao
wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao
wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
Wadau
hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na
Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB
Mkurugenzi
wa idara ya mikopo benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw. Henry Bwogi,
akizoa mada kwa washiriki ambapo alisema, "TPB ndiyo benki kongwe kuliko
zote hapa nchini ikiwa na matawi yaliyosambaa kila kona ya nchi na
hivyo kuwa rahisi kwa wateja kufikiwa na huduma zake, lakini pia benki
hiyo tayari imeonyesha nia ya dhati ya kuwajali wastaaafu ambapo
imekwisha toa mikopo ya mabilioni ya shilingi kwa wanachama wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF.
Bi
Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia vipeperushi
vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo. "Kwa mtu
yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na pensheni au
chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo ili aweze
kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye mifuko ya
kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na uwekezaji wa
namna hiyo kwenye masoko ya fedha.
Bw.
Denis Mwoleka, ambaye ni Meneja wa CRDB tawi la Chuo Kikuu cha SAUT
jijini Mwanza, akizungumza kuhusu umuhimu wa wastaafu hao watarajiwa
kujiunga nabenki hiyo kwa kutarajia kupata faida mbalimbali ikiwemo
huduma mpya ya akaunti ya akiba ya dhahabu ambayo ni njia rahisi ya
kujiwekea akiba ili kufanikisha malengo ya baadaye.
Afisa
kutoka Shirika la viwanda vidogo vidogo SIDO, akihamasisha wastaafu
watarajiwa kuwekeza kwenye uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo
vitawawezesha kujikimu kimaisha na ksutaafu kwa amani. yeye alsiema SIDO
iki tayari kutoa ushauri na mafunzo ya uanzishaji wa viwanda hivyo
Meneja
Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim,(kulia), akifurahia
jambo na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo,
(wapili kushoto) na Meneja Mipango na Utafiti wa Mfuko huo,
Bw.Luseshele Njeje
Meneja
wa Fedha wa PSPF, Bw.Lihami Masoli. (kulia), na Mtafiti Mwandamizi wa
Mfuko huo, Bw.Mapesi Maagi, (katikati), wakibadilishana mawazo na Katibu
Msaidizi wa TSC wilaya ya Kwimba, Bw. Fundikira R.K. James, wakati wa
mapumziko ya semina hiyo
Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim, (kushoto), akifafanua mambo kadhaa kuhusu pensheni
Bw. Silayo (kushoto), akiteta jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi
SHARE
No comments:
Post a Comment