Mtandao wa kutuma
ujumbe kwa njia ya simu wa Telegram, umeahidi kuwa utafunga akaunti
zinazohusiana na ugaidi, baada ya serikali ya Indonesia kufunga huduma
za mtandao huo nchini humo.
Telegram kufunga akaunti za makundi ya ugaidi Indonesiaelegram kufunga akaunti za makundi ya ugaidi Indonesia
Indonesia inadai kuwa Telegram imetumiwa kuunga mkono itikadi kali na kutoa maelekezo ya kufanya mashambulizi.
Mwanzilishi wa mtandao huo amesema kuwa ameghadhabishwa na hatua hiyo.
- IS inavyoeneza taarifa zake
- Islamic State wadai kuendesha shambulizi Mombasa
- Marufuku ya 'Valentine', Indonesia
- Gavana aliyetusi Uislamu afungwa Indonesia
Hatua ya serikali inakuja huku kukiwa na wasi wasi wa kuibuka kwa kundi la Islamic State kusini mashariki mwa Asia.
Kundi hilo limedai kuhusika kwenye mashambulizi kadha nchini Indonesia mwaka huu na limepigana na jeshi mjini Marawi katika kisiwa cha mindanao nchini Ufilipino.
SHARE
No comments:
Post a Comment