Mkurugenzi
Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na
vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania,
lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa
mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya
CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala
Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam
(kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.Mkurugenzi

Salaam.Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT
akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine ni Robert
Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa katika mjadala
huo.Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza
kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo.
Kutoka kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa
ICT pamoja na Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo.Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah akizungumza na washiriki
wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
nchini Tanzania.KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa
mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya
CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni
kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano pamoja na
kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma
hizo. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa
na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo
likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema
wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa
sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa
kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa
watumiaji wa huduma za ICT. Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria
ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila
ya uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na
wasimamizi wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media
itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za
mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi
mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika. Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka ‘Compass Communications Ltd’ akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo.Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza
kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo.
Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.
No comments:
Post a Comment