Jeshi la Australia limepewa nguvu mpya kukabiliana na ugaidi ndani ya nchi.
Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull
Hatua hio mpya inamaanisha kuwa jeshi la Australia litaitwa hivi karibu kusaidia polisi kukabiliana na vitisho.
Hii imetokana na shatuma kuhusu jinsi polisi waliitikia kisa cha ugaidi cha mwaka 2014 mjini Sydney.
Sheria ya sasa inazuia polisi kuwaita jeshi hadi pale watakapohisi kuwa wamelemewa. Chini ya hatua mpya, jeshi pia litatoa mafunzo maalum kwa Polisi.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Waziri mkuu Malcolm Turnbull alisema kuwa anataka kuwepo ushirikiano kati ya polisi na jeshi.
Mateka wawili na mshambuliaji waliuawa wakati wa kisa cha mjini Sydney mapema mwaka huu.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment