Kipa namba mbili wa klabu ya Manchester United Sergio Romero amesaini mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo hadi 2021.
Kipa huyu namba moja wa timu ya taifa ya Argentina amecheza michezo 28 katika misimu miwili aliyoichezea timu yake na katika michezo hiyo ni michezo sita tu aliyocheza katika ligi kuu ya England.
Tetesi za golikipa namba moja wa Man United, David De Ge kuwa anaweza kusajiliwa na Real Madrid, huenda zikawa zimechangia kwa kipa huyu kuongeza mkataba mpya.
SHARE
No comments:
Post a Comment