NA K-VIS BLOG, DODOMA
SHINDANO la ngoma za utamaduni liitwalo ‘Mavunde na utamaduni
wetu’ limefanyika mjini Dodoma likiwa na lengo la kuenzi, kulinda na
kuhifadhi utamaduni wa watu wa Dodoma.
Shindano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma
mjini Anthony Mavunde(pichani juu katikati), na lilihusisha vikundi vya ngoma za asili ya Dodoma 7.
Vikundi hivyo ni Simba dume, changamoto, Noti mtemi, Neema
Yerusalem, Chipukizi, Finga Vikonje na Imani Makulu.
Akizungumza katika shindano hilo, Mbunge wa Dodoma Mjini
Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema
uwepo wa shindano hilo ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa
kampeni za uchaguzi Mkuu 2015 na kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli
kwa kuhamishia shughuli za serikali Dodoma, kupiga vita Rushwa na Ubadhirifu na
Kulinda Maliasili za Taifa kwa manufaa ya watanzania wote.
“Tamaduni zetu zilikuwa zimeanza kusahaulika watu hawakuona tena
umuhimu wa ngoma za jadi na hii ni kutokana na utandawazi na kuwa watu wa mjini
sana tumesahau tumetoka wapi,”amesema Mavunde
Amebainisha katika kampeni hizo aliahidi kwa nafasi yake
atajitahidi kuviunganisha vya kutoka maeneo mbalimbali ili kuenzi na kulinda
utamaduni wa Dodoma.
“Hatua yetu ya kwanza ni kukusanya vikundi na kuvipambanisha
lakini baadaye tutakuwa na makubwa ya kimkoa kila mwaka na hii nawashawishi na
wenzangu pia, ili mkoa wetu uendelee kutunza na kuhifadhi utamaduni
wetu,”amesema
Mavunde amesema shindano hilo linalenga kuwakumbusha vijana kuwa
mababu zao waliishi kwa namna gani.
Kwa upande wake, Chifu wa Dodoma mjini Lazaro Chihoma
amempongeza mavunde kwa kuandaa tamasha hilo na kudai kuwa wamepita viongozi
wengi lakini hawakuona umuhimu wa kuenzi utamaduni wao.
Vikundi vilivyoibuka kidedea ni pamoja na kikundi cha Imani
Makulu ambacho kimepata kombe na fedha Sh.300,000, mshini wa pili ni Kikundi
cha Chipukizi kimepata Sh.250,000 na ngao na mshindi wa tatu Figa Vikonje
kimepata Sh.150,000 huku vingine vikipatiwa Sh.80,000 kila kimoja.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde, ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini (CCM), akizungumza
katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu lililofanyika mjini Dodoma.
Chifu wa Dodoma mjini Lazaro Chihoma akizungumza katika Shindano
la Mavunde na Utamaduni wetu, mjini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akiwa na
viongozi mbalimbali katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
Umati wa wakazi wa Dodoma waliohudhuria shindano la Mavunde na
Utamaduni wetu.
Umati wa wakazi wa Dodoma waliohudhuria shindano la Mavunde na
Utamaduni wetu.
Moja ya vikundi vya ngoma za kiasili vilivyoshiriki katika Shindano la
Mavunde na Utamaduni wetu.
Moja ya vikundi vya ngoma za kiasili vilivyoshiriki katika Shindano la
Mavunde na Utamaduni wetu.
SHARE
No comments:
Post a Comment