TAARIFA KWA UMMA: DAWASCO KUKATA MAJI KUANZIA AGOSTI 14-19, 2017
UBORESHAJI WA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI
BAGAMOYO MKOANI PWANI.
Shirika
la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wateja
wake wote wa Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji
wa Ruvu Chini utakuwa kwenye maboresho kwa wastani wa siku 5, kuanzia
siku ya Jumatatu tarehe 14/08/2017 hadi 19/08/2017, hivyo kusababisha
baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo kuwa na upungufu wa kiwango cha
huduma ya Majisafi.
Sababu
ya upungufu wa Majisafi: Maboresho ya Mtambo na mabomba makuu ya
usafirishaji na usambazaji Maji.Maeneo yatakayoathirika: Mji Wa Bagamoyo
Vijiji Vya Zinga, Mlingotini, Kilomo na Mapande.
Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha kuepuka adha itakayojitokeza.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia:
Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) au
Dawati la huduma kwa wateja Dawasco Bagamoyo 0743 451 887
www.dawasco.go.tz
Imetolewa Na:
Ofisi Ya Uhusiano
Dawasco-Makao Makuu.
SHARE
No comments:
Post a Comment