Msanii wa hip hop Bongo, Nikki Mbishi amempa pongezi msanii Roma kwa wimbo wake mpya ‘Zimbabwe’.
Rapper
huyo amesema ngoma hiyo ndani ya siku mbili kupata viewers zaidi
450,000 katika mtandao wa YouTube ni ishara ya kufanya vizuri na ni
mafanikio katika level ya muziki wa hip hop hususani Tanzania.
Nikki
ameendelea kueleza kuwa alipoona ngoma hiyo kwa mara ya kwanza
alishawishika na ikabidi atumia MB zake kwa ajili ya kudownload na
alipoupa na kuusikiliza alishtuka kidogo na kuhisi mbona kama jamaa kuna
kitu anataka kukisema.
“Nikagundua
maswali mengi siku ambao waandishi wa habari walikwenda na makamera
kwenda kuhoji pale lakini yale maswali waliyomuuliza Roma siyo ambayo
yalitakiwa aulizwe na ambayo waliulizwa hayakujibiwa, lakini Roma
amefanikiwa japo kwa kifupi kuyajibu kwenye wimbo, kwa hiyo ni kile kila
mtu alikuwa anatamani kujua,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na
kuongeza.
“Sijui
ripoti ya utekaji ameiteka mtekaji na vitu kama vile, then anawashukuru
watu waliotabiri atatoka jumapili kwa kuwa kuna manabii wametabiri
kwamba mwanenu amepotea lakini jumapili atakuwa amepatikana ni vitu
ambavyo ni live yeye kaviongea, me naona alichosema ni kizuri,” amesema
Nikki.
Pia
Nikki amesema wimbo haupo negative tu kwamba Roma anaipinga serikali
kwani kamsifia Mh. Rais Dkt. Magufuli kwa kujenga bomba la mafuta kutoka
Uganda hadi Tanga.
SHARE
No comments:
Post a Comment